MKASA MZIMA ULIKUWA HIVI.....
Mwanamke mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mke wa mtu anateseka hospitalini
baada ya kuchomwa na mafuta ya kupikia ya moto na ndugu yake baada ya
kuhisiwa kuiba vocha ya simu ya mtandao wa Telecel yenye thaman ya senti
50 huko Zimbabwe.Kijana
huyo aliyejulikana kwa jina la Otilia Kosa anayeishi Plot 16, Tsungwizi
Ridge maeneo ya Nyazura huko nchini Zimbabwe anateseka katika hospitali
ya Rusape General Hospital akiuguza majeraha aliyoyapata baada ya
kumwagiwa mafuta ya moto na ndugu yake.
Inadaiwa kwamba mnamo tarehe 27
Decemba 2013, Otilia alimuuliza ndugu yake Kudakwashe kama yeye ndiye
aliyetumia vocha yake ya mtandao wa Telecel yenye thamani ya senti 50 za
kizimbabwe.Kudakwashe alikataa kuwa hakutumia vocha hiyo na hapo ndipo
mtafaruku mkubwa ulipotokea kati ya wawili hao.
Cha
kushangaza ,siku iliyofuata kikao cha familia kilikaa ili kuwapatanisha
wawili hao ambao walishindwa kuelewana na mpaka kufikia hatua mbaya
ambayo ingepelekea kuvunja udugu wao.Hata hivyo, wanafamilia hao
walishindwa kuwapatanisha ndugu hao na hivyo kuongeza mpasuko kati yao.
Ilidaiwa
kuwa baada ya kukosa muafaka huo,Kudakwashe alipatwa na hasira kali
iliyompelekea yeye kuingia jikoni na kuchemsha mafuta ya kupikia na
kummwagia nduguye huyo (Otilia) katika maeneo ya uso,shingo,kifua,mikono
na tumboni.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Afisa wa Polisi wa ZRP Nyazura, Inspekta hikima
Sanida alinukuliwa akisema "We have arrested the suspect and recorded a
warned and cautioned statement in which she admitted scalding the victim
with hot cooking oil. She was charged with first-degree assault and
criminal violation of the Domestic Violence Act,"
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
No comments:
Post a Comment