Dar es Salaam. Uchafu unaotupwa baharini hasa wa mifuko ya plastiki ndiyo uliosababisha kuzima ghafla kwa injini ya Kivuko cha Mv Magogoni katikati ya wiki hii.
Akizungumza jana kuhusu hali hiyo, Meneja
Mawasiliano wa Sumatra, David Mziray alisema kuwa mafundi baada ya
kuchunguza injini nne za kivuko hicho, walibaini kwamba zimejaa taka.
“Propela zilivuta maji yenye uchafu mbalimbali na hivyo injini
zikashindwa kufanya kazi vizuri. Mafundi walitoa uchafu wakaifanyia
marekebisho na kuijaribu kwa dakika kama 20,” alisema Mziray.
Alisema kuzima ghafla kwa injini kulizua hofu
kubwa kwa abiria, ingawa hawakuwa katika hali ya hatari kwa sababu meli
ikizima katikati ya maji haizami.
“Tumebaini kuna haja ya kutoa elimu ya usafiri wa majini kwani hofu ya abiria ingeweza kusababisha maafa makubwa.CHANZO MWANAINCHI
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,PIA BOFYA HAYO MATANGAZO UNAYOYAONA KUJIFUNZA VITU VINGI(USIPITWEEEEEEEE)
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,PIA BOFYA HAYO MATANGAZO UNAYOYAONA KUJIFUNZA VITU VINGI(USIPITWEEEEEEEE)
No comments:
Post a Comment