Longido.Serikali imeshauriwa kuanza mchakato wa kuunda Katiba ya Serikali ya Tanganyika ili iweze kuendana na matakwa ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakizungumza katika semina ya mashirika yasiyo ya
Kiserikali Mkoa wa Arusha iliyoandaliwa na Chuo cha Uongozi na Maendeleo
cha MS-TCDC na Mtandao wa taasisi zisizo la kiserikali mkoani Arusha
(ANGONET), watendaji wa mashirika hayo walibainisha kuwa ili Jamhuri ya
Muungano iwepo ni muhimu kurejea Serikali ya Tanganyika.
“Huwezi kuwa na Katiba ya Muungano, wa Serikali ya
Zanzibar bila kuwa na Serikali ya Pili, hivyo ni muhimu sasa kuanza
mchakato ya kuandikwa Katiba ya Tanganyika,” alisema Elibariki Malley.
Malley ambaye pia ni Diwani wa Arusha, alisema ni
vyema sasa wakati mchakato wa Katiba Mpya umeanza, zianze taratibu za
haraka kupata Katiba ya Tanganyika ambayo itakuwa ni tofauti na Katiba
ya Jamhuri,” alisema
Akitoa mada juu ya katiba katika semina hiyo,
Mkufunzi Mshiriki wa Chuo cha MS-TCDC, Mwanasheria, Anna Mghwira alisema
kuwa katika rasimu ya Katiba Mpya, Tanganyika haikutajwa wazi bali
imetajwa Tanzania Bara.CHANZO MWANAINCHI
No comments:
Post a Comment