Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, December 17, 2013

waandishi wa habari watakiwa kuendelea kuelimisha jamii juu ya Ukimwi


TACAIDS_2_a188c.jpg
MAGRETH KINABO-MAELEZO- Dar es salaam
Vyombo vya habari hapa nchini vimetakiwa kuwa na kampeni za kuelimisha jamii kuhusu mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vinavyosababisha UKIMWi kuwa za kudumu ili kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo kwa vijana na wanawake.
Kauli hiyo imetolewa jana (jana) jijini Dar es salaam na Mwenyekiti Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za UKIMWI(AJAAT) Simon Kivamo wakati wa hafla fupi ya utoaji wa zawadi kwa waandishi wa habari waliofanya vizuri katika shindano la makala za UKIMWI liliandaliwa na AJAAT kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS).
Alisema kuwa katika shindano la mwaka huo lilenga kuelimisha wananchi kuhusu madhara ya VVU na UKIMWI kwa wanawake na vijana ili kupunguza vifo kwenye kundi hilo vinavyotokana na maambukizi ya ugonjwa huo.
Kivamo aliongeza kuwa washindi walitakiwa pia kuchambua ni kitu gani kifanyike katika kuzuia makundi hayo mawili ya wanawake na vijana dhidi ya maambukizi mapya na hatimaye kuwa na familia bora na taifa imara kwa ujumla.
Katika shindano hilo washindi wa walizawadiwa vyeti na fedha taslimu ni Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Raymond Kaminyonge alipata zawadi ya Sh. 500,000akiwa ni mshindi wa kwanza, wa pili ni Hellen Ngoromera wa gazeti la Tanzania Daima(350,000) na Peter Muthamia wa The Citizen alipata Sh. 300,000.
Washindi wengine waliopata Sh. 250,000 kila mmoja ni Husna Mohammed wa Zanzibar Leo, Gerald Kitabu wa The Guardian, Eben – Ezey Mende wa Jambo leo na Rehema Mohammed wa Majira.
Kwa upande wa Radio na Luninga ,washindi waliopata fedha na vyeti ni Magret Tengule wa Star TV aliibuka mshindi wa kwanza aliyepata Sh. 500,000 na wa pili Rahabu Fred alipata Sh. 300,000. Pia mchora vibonzo wa gazeti la Nipashe Abdul Kingo alipata Sh. 500,000.Waandishi wengine 18 walioshiriki walipata vyeti pekee.
Akizungumza kabla ya kuwakabidhi washindi hao zawadi Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi wa TACAIDS,Jummane Isango aliishauri jamii kuhakikisha inajikinga na ugonjwa huo kwa kuwa 'Tanzania bila Ukimwi inawezekana'.
Hivyo kila mmoja akitimiza wajibu wake ifikapo mwaka 2015 maambukizi ya ugonjwa huo na vifo yatakuwa ni asilimia zero.



No comments:

Post a Comment