-AMA KWELI MGANGA HAJIGANGI
WANAFUNZI
wanaosomea udaktari katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili (Muhas) wanaishi katika mazingira hatarishi kwani wanaweza
kupata magonjwa ya mlipuko na yale ya kuambukizwa wakati wowote.
Uchunguzi
uliofanywa na Operesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ndani
ya majengo ya chuo hicho yaliyo karibu na taasisi ya mifupa (MOI),
umegundua kwamba kwa miezi mingi, vyoo vinavyotumiwa na wanafunzi hao
vimejaa na kuziba kabisa, hali inayowafanya vijana hao, licha ya
kushindwa kupata huduma hiyo muhimu ya kibinadamu, pia kuwa katika
hatari ya kupatwa na magonjwa ya mlipuko.
“Hali ni
mbaya sana hapa kwa kweli. Hatuna huduma ya choo kwa miezi miwili hadi
mitatu sasa, tunapobanwa na haja, hasa kubwa, hulazimika kukimbilia
Kariakoo kwenye vyoo vya kulipia, hapa hapafai,” mmoja wa wanachuo hao
aliiambia OFM na kuomba hifadhi ya jina lake.
Wanafunzi
hao ambao walitoa ushirikiano wa kutosha kwa makachero wetu, pia
walisema majengo mengi yanayotumiwa kama mabweni yao ya kulala,
yamechakaa na hivyo kuwafanya wawe na hofu kubwa, kwani yanaweza
kuanguka wakati wowote.
OFM
ilishuhudia ngazi za kushuka na kupanda, zinazozunguka nje ya majengo
hayo zikiwa zimechakaa vibaya huku vyuma vilivyowekwa pembeni kwa ajili
ya kujishikilia vikiwa vimemongonyoka. Ni hatari kama likitokea tukio la
ghafla, mfano wa moto, litakuwa ni jambo gumu kwao kuweza kujiokoa
kupitia ngazi za nje. Hata baadhi ya milango inayotokeza nje ya ngazi
hizo katika maghorofa hayo, imefungwa kutokana na ubovu.
Licha ya
kero hizo, pia wanafunzi hao walilalamikia kitendo cha kujazana kupita
kiasi katika vyumba vyao vya kulala, kwani wamepangwa hadi wanane katika
chumba kimoja.
Baada ya
kutoka kwenye chumba cha madenti hao (majina tunayo) OFM ilitua kwenye
jengo moja ambalo liliwahi kulipuka kwa moto lakini bado limechakaa
kutokana na kutofanyiwa ukarabati.
MSEMAJI WA MUHIMBILI ABANWA, AKISALITI CHUO
Baada ya OFM kunasa uozo huo ndipo ilipoamua kuwasiliana na msemaji wa Muhimbili, Amiela Angelekera.
OFM: Habari za leo kiongozi?
AMINIELA: Salama tuu, za kwako? Samahani naongea na nani?
OFM: Unaongea na Operesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers.
AMINIELA: Ok, nikusaidie nini?
OFM:
Unafahamu kama vyoo vya hosteli ya wanafunzi vyote vimejaa? Je, kuna
mkakati wowote wa kurekebisha maana ni miezi mingi imepita.
AMINIELA:
Mmmh..(anaguna kidogo) sijajua ni vyoo vipi, unatakiwa uwe mwandishi
mzuri wa taaluma yako unapozungumzia chuo, njoo twende wote tukaone
hivyo vyoo.
OFM:
Taaluma ipi ambayo unadhani hawana OFM? Tayari tumefika hapo na kujionea
ubovu wa miundombinu ambayo inahatarisha maisha ya wanafunzi na chuo
kwa ujumla.
AMINIELA:
Nimesema njoo ofisini kwangu, maana sipendi kuzungumza kwenye simu ishu
kama hizi, kwanza mimi sihusiki na chuo maana ni taasisi nyingine.
OFM: Ok, kwa nini umelizungumzia suala hilo.
AMINIELA: Sihusiki na chuo, hiyo ni taasisi nyingine.
OFM: Ok, sawa kazi njema.
source: GPL
No comments:
Post a Comment