Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, December 31, 2013

AMBULANCE’ NUSURA ICHOMWE MOTO SUMBAWANGA NA WANAINCHI.

Wananchi waliotaka kujichukulia sheria mikononi, nusura walichome moto gari la wagonjwa lilitolewa msaada Kituo cha Afya Mtowisa wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa kutokana na madai ya kuchangia kifo cha mwalimu mmoja aliyekosa msaada wa haraka wakati wa kujifungua.
Wananchi hao wanadaiwa kulishambulia gari hilo kwa mawe na kuvunja moja ya kioo.
Gari hilo linadaiwa kuchelewa kuja kumchukua Mwalimu Leah Mgaya wa Shule ya Msingi Mtowisa 'A', ambaye alifariki baada ya kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua.
Habari kutoka sehemu ya tukio zilizothibitishwa na Ofisa Tarafa ya Mtowisa, Peter Masindi zinaeleza kuwa, awali mwalimu huyo alipelekwa katika kituo hicho cha afya juzi saa 3 asubuhi akiwa katika hali uchungu wa kujifungua, lakini baadaye ilionekana anahitaji kupewa rufaa kwenda Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini hapa.
Masindi alisema kutokana na hali hiyo ililazimu kupiga simu Ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya saa 6 mchana ili kuomba msaada wa gari, lakini gari hiyo ilichelewa kufika kutokana na kudaiwa ilisafiri kwenda wilayani Nkasi, na hata iliporejea jioni ilikwama njiani kutokana na hali ya mvua.
Mmoja ya wananchi waliozungumza na gazeti hili, Mwaipungu alisema kifo cha mwalimu huyo kiliwakera wananchi wa eneo hilo, ambapo walikusanyika kwenye makundi na kuanza kujadiliana.
Wananchi hao walidai kuwa gari hilo la wagonjwa halina msaada kwani muda mwingi haliko kituoni hapo hivyo kutaka kulichoma moto.
Hasira za wananchi hao zilionekana baada ya kufika kwa dereva wa gari hiyo aliyefika, huku akiliza king'ora lakini alipokelewa kwa mabango, kabla ya kumsimamishwa kumtaka kuwapa funguo za gari, jambo lililopingwa na dereva. huyo huku wananchi hao wakilishambulia kwa mawe.

No comments:

Post a Comment