Baadhi wa wazazi katika Hospitali ya Mwananyamala. |
Watoto
124 wakiwemo wa kiume 80 wamezaliwa katika mkesha wa Sikukuu ya Krismasi
katika hospitali za Dar es Salaam huku wengi wakiwa wa kiume.
Watoto
hao wamezaliwa katika hospitali za Muhimbili, Temeke, Mwananyamala na
Amana, ambapo watoto wanne katika hospitali ya Mwananyamala walizaliwa
kwa njia ya operesheni.
Mganga wa
Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk Sophinias Ngonyani alisema
watoto waliozaliwa katika hospitali hiyo jumla walikuwa watoto 42,
ambapo 18 wakike na 24 wakiume .
Ngonyani alisema kuwa hakuna mtoto au mama aliyepoteza maisha katika mkesha wa Krismasi.
Katika hospitali ya Amana, walizaliwa watoto 38, ambao wakike 12 na wakiume 26.
Kwa
upande wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, watoto waliozaliwa ni sita, huku
kukiwa hamna aliyezaliwa kwa njia ya upasuaji. Hospitali ya Temeke
jumla ya watoto waliozaliwa ni 38, ambapo wakiume ni 24 na wa kike ni
12.
Muuguzi
wa zamu wa hospitali ya Temeke, Happiness Mbalawa alisema watoto
waliozaliwa kwa njia ya upasuaji hospitalini hapo ni wawili, wakiume
mmoja na wakike mmoja.
Katika hospitali zote hakuna mtoto aliyepoteza maisha au kuzaliwa na ulemavu.
No comments:
Post a Comment