
Na Heri Shaaban
Wizara ya
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, limetoa mwezi mmoja kwa watumishi wake
wote kuwasilisha vyeti vyao ili viweze kufanyiwa uhakiki ili kubaini
kama kuna vyeti feki.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Job Masima, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati wa Mafunzo ya Elimu ya Hifadhi ya Jamii yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).
Alisema kuanzia leo,
watumishi wote waliopo chini ya Wizara hiyo watapaswa kuwasilisha vyeti
vya vyuo walivyosomea."Natoa mwezi mmoja kuanzia leo hadi Januari,
wawasilishe yeti vyao wizarani viweze kukaguliwa...baada ya ukaguzi
tutafuatilia maeneo waliyosomea ili kubaini kama kuna
askari wanaotumia vyeti feki," alisema.
Alisema askari ambao
watabainika kutumia vyeti feki na kupata vyeo wakiwa kazini, watashushwa
vyeo ambapo lengo a ukaguzi huo ni kuwataka watumishi hao kusomea
katika vyuo vinavyotambulika na Serikali si vya mitaani.
Aliongeza kuwa, mpango huo
pia utawahusisha watumishi ambao wamesomeshwa na Wizara ambao nao
watatakiwa kwasilisha vyeti vyao upya.Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu
wa SSRA, Bi. Irene Isaka, aliwataka watumishi wa Wizara hiyo kujiunga na
Mifuko ya Hifadhi za Jamii kwa ajili ya kuweka mafao yao.
Alisema kuna mifuko mingi
hivyo kila mtumishi anaweza kuchagua wowote anaopenda kujiunga nao ili
uweze kumsaidia dhidi ya matukio yasiotarajiwa.Matukio hayo ni pamoja na
maradhi, ulemavu, kustaafu kazi,kuacha kwa hiari au kwa lazima.
Akizungumzia changamoto zilizopo katika sekta hiyo, alisema takwimu
zinaonyesha wananchi walio katika sekta rasmi wanakadiriwa kufikia
milioni 1.5 ndio wananufaika na sekta hiyo.
Majira


No comments:
Post a Comment