MABINGWA
watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Yanga ya Dar es
salaam leo hii i ndani ya uwanja wa Taifa inashuka ugani kucheza mechi
ya kirafiki dhidi ya maafande wa KMKM kutoka visiwani Zanzibar ikiwa ni
maandalizi ya mechi yao ya kuhitimisha kampeni ya Nani Mtani Jembe,
desemba 21 mwaka huu.
Mechi
hiyo itakuwa maalum kwa benchi la ufundi la klabu hiyo chini ya kocha
mkuu, Ernie Brandts akisaidia na Fredy Minziro kuwapima vijana wao kabla
ya kula sahani moja na Mnyama Simba.
Kuelekea
katika mechi hiyo, maandalizi yote yamekalika na baada ya mechi ya leo,
nao Wekundu wa Msimbasi Simba watashuka dimbani kesho kuwakabili KMKM
katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.Simba na Yanga
zinajiandaa na pambano la `KAMPENI YA NANI MTANI JEMBE`ambalo ni zawadi
ya kufungia mwaka kwa mashabiki na kila timu imetia sahihi makubaliano
kwamba itachezesha kikosi cha kwanza ili kuwapa mashabiki burudani ya
uhakika.”
Hivi
karibuni, Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema
kuwa mechi hii ni maalum kwa ajili ya kuhitimisha kampeni ya Nani Mtani
Jembe ambayo imeendeshwa kwa zaidi ya miezi miwili ikiwapa fursa
mashabiki wa timu hizi kuchangia timu zao kila wanapoburudika na bia ya
Kilimanjaro Premium Lager.
Kilimanjaro
Premium Lager ilitenga kiasi cha shilingi milioni 100
zinazoshindaniwa na Simba na Yanga kupitia mashabiki wake na tarehe 21
Desemba ndio utakuwa mwisho wa kampeni ya Nani Mtani Jembe ambapo baada
ya mechi fedha hizo zitagawanywa kwa kila timu kulingana na matokeo ya
kura za mashabiki na klabu zitajiamulia namna ya kutumia fedha hizo.
Kuelekea
katika pamano hilo la mechi hiyo, kocha msaidizi wa Yanga, Fredy Ferlix
Minziro, `Katalaiya Majeshi, Baba Isaya` amesema vijana wote wapo
salama, morali yao ni kubwa sana kuelekea kuwakabili Simba Sc.
“Ni
nafasi nyingine kwa vijana wetu kuonesha uwezo wao mkubwa mbele ya
Simba baada ya sare ya 3-3 katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania
bara”. Alisema Minziro.
Minziro
alitamba kuwa Simba walimshukuru sana Mungu baada ya sare ya 3-3,
lakini mtihani mwingine mgumu kwao umekaribia ukizingatia wao Yanga ni
bora kuliko wao.
“Kutoka
nyuma kwa mabao 3-0 na kusawazisha na hatimaye kupata sare ya 3-3
ilikuwa bahati yao na walimshukuru sana Mungu. Desemba 21 wanaingia
uwanjani wakiwa na mchecheto mkubwa kwani wanafahamu wazi kazi yetu
ilivyo bora”. Alijigamba Minziro.
Kuelekea
mechi hiyo, Yanga wataingia uwanjani wakiwa na wachezaji wapya, Juma
Kaseja na Hassan Diliunga ambao wamethibitishwa kupewa mikataba na klabu
hiyo.
Kwa
upande wa Simba, wao wataingia wakiwa na wachezaji kadhaa wapya
wakiwemo makipa Ivo Mapunda, Yaw Berko, kiungo Awadh Issa Juma kutoka
Mtibwa, beki kutoka Gor Mahia ya Kenya, Donald Mosoti Omwanwa na
wengine.
Pia
wataingia uwanjani wakiwa na makocha wapya, Mcroatia, Zdravko Logarusic
akisaidiwa na msaidizi wake ambaye ni kiungo wa zamani wa klabu hiyo na
aliyekuwa kocha wa timu ya Simba B, Seleman Matola `Veron`.
Kwa
mazingira hayo, benchi la Ufundi la Simba SC litahitaji kutafuta
ushindi ili kujenga imani kwa mashabiki wao wenye machungu ya kuzidiwa
na watani zao wa jadi, klabu ya Yanga, wakati Yanga wataingia na sura
zilezile za benchi la ufundi.

No comments:
Post a Comment