Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, July 5, 2013

HAYA SASA HILI NDO BAFU LA AUTOMATIC LITAZAME HAPA

Automatic Shower pictures

MAGUFULI::NINAUTAMANI URAIS..

.
Katika hali inayoonyesha kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, anautamani urais, amesema anaweza kutangaza nia hiyo kama atakidhi masharti yatakayowekwa kwenye Katiba mpya.
Alisema iwapo Katiba ijayo itakuja na sifa ambazo atakidhi vigezo kuna uwezekano mkubwa wa kuwania nafasi hiyo na kwamba iwapo atapungukiwa sifa zinazohitajika kwa mujibu wa Katiba hataingia kwenye kinyang’anyiro hicho.
Dk. Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wazee wa
wilaya hiyo kwenye ukumbi wa ‘Mshikamano Saccos’, muda mfupi baada ya mzee Paschal Nyambibo (87) kumsihi agombee nafasi hiyo mwaka 2015 kutokana na sifa zake za uchapakazi ndani ya serikali.
Nyambibo alisema kutokana na uwajibikaji mzuri aliouonyesha Dk. Magufuli tangu mwaka 2000 akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na katika wizara mbalimbali, Watanzania wamekuwa na imani kubwa na uwajibikaji wake na kwamba anastahili kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ifikapo mwaka 2015.
Licha ya kauli hiyo kusababisha minong’ono mingi kwa wazee waliohudhuria kikao hicho, Dk. Magufuli alionekana kutuliza hali hiyo kwa kusema isubiriwe Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano iwapo itakuwa na masharti ambayo yatamfanya kujitathimini iwapo ana sifa za kugombea au vinginevyo.

Hata hivyo, Dk. Magufuli hakusita kuonyesha hisia zake za kukerwa na baadhi ya wananchi wanaobeza maendeleo aliyotekeleza katika jimbo lake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge.
Alimshutumu hadharani aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Chato kabla ya kuhamishiwa wilayani Mbogwe, Gervas Stephano, kuwa hana shukrani.
Dk. Magufuli alimwelezea katibu huyo kuwa hana fadhila kutokana na mambo mengi aliyomtendea tangu akiwa katibu wa ofisi yake ya jimbo ambapo alimsaidia kupanda ngazi na kuwa Katibu wa CCM wilaya Chato, Kwimba, Kasulu, Kilosa na kurejea tena Chato kabla ya kuhamishiwa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita  kuendelea na wadhifa huo.
“Tatizo lenu watu wa Chato hamna shukrani…mambo mengi nimefanya hapa Chato, lakini yote mnaona ziro…hata niliowasaidia kama Gervas naye sasa hivi ananiponda…lakini nawashukuru sana wazee wangu kwa kunikumbusha niliyoyafanya kwenye jimbo letu kupitia risala yenu nzuri,” alisema Dk. Magufuli.
“Kutokana na hali hiyo ninawazawadia Sh. 1,000,000 mfanye sherehe ya kujipongeza kwa kuwa natambua mmejitesa sana mpaka kufanikisha kikao hiki cha leo…na kwa kuwa hamna mradi wowote wa kuwaingizia kipato kama wazee, ninaahidi kuwapa Sh.   3,000,000 kutoka mfuko wa jimbo, ili muanzishe walau saccos ya kukopeshana,” alisema.
Baadhi ya viongozi na wananchi wamekuwa wakilitaja mara kwa mara jina la Waziri Magufuli miongoni mwa watu wanaodhaniwa kutaka kugombea nafasi ya urais wa Tanzania mwaka 2015, ingawa mwenyewe amekuwa akikanusha uvumi huo.
Mbali na Dk. Magufuli, wengine ndani ya CCM wanaotajwa  ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa; Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye anajiita mtaji wa urais; Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Ushirikiano wa Kimataifa –CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Mambo ya Nje, Bernard Membe, ambaye alipata kusema anasubiri kuiteshwa na Mungu kuwania nafasi hiyo.

SOURCE: NIPASHE

SOMA ALICHOKISEMA MWANA FA KUHUSU NYIMBO MPYA YA GODZILLAH


Rapper MwanaFA, mapema jioni hii ameisifia ngoma mpya ya rapper mwenzie, Godzilla “THANK YOU” ambayo ameiachia masaa kadhaa yaliyopita …
Kupitia mtandao wa kijamii wa twitter, @MwanaFA alitweet, “Mi sijui nyi mnaonaje lakini hii ngoma ya Zilla na Walter ingeweza tu kuingia kwenye MCHG na ikaenea … Ndo nshasema hivo … #Bye “
MCHG ni short form ya album mpya ya Jay-Z “MAGNA CARTA HOLY GRAIL” iliyoachiwa masaa machache pia na kila mtu kuisifia ni kali … MwanaFA amei-rank ngoma mpya ya King Zilla “THANK YOU” kwa ukali wake na kusema kuwa inaweza kufit kabisa ndani ya album hiyo ya mkali wa Hip Hop duniani kwa sasa …
Zilla amefanya ngoma hiyo na Walter ambapo imetengenezwa na Prod. Marco Chali (MJ Records)

RAIS MSTAAFU ALHAJI ALI HASSAN MWINYI AWASILI LEO HII JIJINI WASHINGTON DC MAREKANI, KAMA MGENI RASMI WA TAMASHA LA KISWAHILI NCHINI MAREKANI


 Rais Mstaafu Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles.
 
Rais Mstaafu Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiwa ameambatana na Mkewe mama Siti Mwinyi, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles.

Na Alex Kassuwi/Swahili TV
 
Rais Mstaafu Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi awasili leo hii katika jiji la Washington DC, Marekani, ambapo atakuwa mgeni rasmi katika tamasha la kukienzi na kukikuza kiswahili nchini  Marekani. Tamasha hili ambalo limeandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani litafanyika kesho kutwa siku ya Jumamosi tarehe Julai 6, 2013 katika Ukumbi wa mikutano wa Hampton uliopo katika Jimbo la Maryland.
 

Kutoka kushoto, Afisa Ubalozi Bw. Suleiman Saleh, Mama Siti Mwinyi, Rais mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi na Kaimu Balozi Bi. Lily Munanka, mara baada ya kumpokea Mgeni Rasmi katika Tamasha la Kiswahi chini Marekani litafanyika kesho kutwa siku ya Jumamosi tarehe Julai 6, 2013 katika Ukumbi wa mikutano wa Hampton uliopo katika Jimbo la Maryland.

 
Picha kutoka kuchoto; Mkurugenzi wa Swahili TV Bw. Alex Kassuwi. Mama Siti Mwinyi, Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Kaimu Balozi Bi. Lily Munanka, mara baada ya kumpokea Rais Mstaafu Mwinyi.
 

Gari lililombeba Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi lilikielekea katikati jiji la Washingston DC, Marekani, leo hii Julai 4, 2013
Msafara wa  Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi ukielekea katikati jiji la Washingston DC, Marekani, leo hii Julai 4, 2013
 

Hoteli alikofikia  Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi katika jiji la Washingston DC, Marekani, leo hii Julai 4, 2013
Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan akipokelewa na mtoto aliyempa ua katika hoteli yake Washingston DC, Marekani, leo hii Julai 4, 2013

Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kuwasili katika hoteli yake Washingston DC, Marekani, leo hii Julai 4, 2013
 
Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiongea na wenyeji wake mara baada ya kuwasili katika hoteli yake Washingston DC, Marekani, leo hii Julai 4, 2013
 

Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bw. Iddi Sandali  akiwa na Kaimu Balozi Bi. Lily Munanka
 

Emmanuel Mgaya aka Masanja Mkandamizaji akiwa na Mkurugenzi wa Swahili TV Bw. Alex kassuwi katika Hoteli alikofikia

Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi leo hii Julai 4, 2013
 
 
Shilole akiwa na Mkurugenzi wa Swahili TV Bw. Alex kassuwi  katika Hoteli alikofikia

Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi leo hii Julai 4, 2013

 
Dr. Amour Mwinyi akiwa na mdau katika Hoteli alikofikia
Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi leo hii Julai 4, 2013
 

 Bi. Mindi Kasiga, Afisa habari wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani akiwa na Mkurugenzi wa Swahili TV Bw. Alex kassuwi katika Hoteli alikofikia
Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi leo hii Julai 4, 2013
 
Msanii Shilole akiwa na wadau waliokuja kumpokea 
Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi leo hii Julai 4, 2013 katika Hoteli yake.

 Mfanyakazi wa Ubalozi Bw. Eliud Mbowe  akiwa na Mkurugenzi wa Swahili TV Bw. Alex kassuwi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani leo hii Julai 4, 2013
 
 Bi. Asha Nyang'anyi akiwa na wadau  katika Hoteli alikofikia
Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi leo hii Julai 4, 2013
 
 Wadau waliofika katika Hoteli alikofikia
Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi leo hii Julai 4, 2013
 
 Masanja akiwa na shabiki wake katika Hoteli alikofikia
Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi leo hii Julai 4, 2013

POLISI WAVAMIA NYUMBANI KWA MJUKUU WA MANDELA KUSAKA MABAKI YA MIILI...


KUSHOTO: Mandla Mandela. KULIA: Msafara wa maofisa wa polisi pamoja na gari la kubebea maiti wakielekea kusaka miili nyumbani kwa Mandla huko Mvezo.
Polisi wa Afrika Kusini wamevamia nyumbani kwa mjukuu wa Nelson Mandela kusaka miili mitatu anayodaiwa kuihamisha kinyume cha sheria.
Hii imekuja baada ya Mandla Mandela juzi kushindwa kesi mahakamani dhidi ya ndugu 16 wa familia yake ambao wanamtuhumu kwa kuhamisha miili hiyo ya watoto watatu wa rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini bila idhini yao.

Mahakama ya Mthatha iliamua kwamba mabaki hayo yarejeshwe katika eneo ya maziko la familia hiyo hadi kufikia juzi Saa 9 alasiri.
Askari wa Mahakama walivamia milango ya kuingia nyumbani kwake huko Jimbo la Eastern Cape nchini Afrika Kusini wakiwa na mashoka kabla ya maofisa wa polisi kufukua ardhini kusaka miili hiyo. Magari matatu ya kubebea maiti mazikoni pia yalionekana kwenye eneo hilo, gazeti la Eyewitness News la Afrika Kusini liliripoti.
Familia hiyo ilimburuta Mandla mahakamani baada ya kuzika upya mabaki ya miili katika eneo lake alikozaliwa la Mvezo mwaka 2011.
Ndugu wa Mandela walidai kwamba Mandla hakuwa na ruhusa au hata kuwataarifu wanafamilia wakati akifanya maamuzi hayo.
Ndugu wa Mandla wamesema kwamba nafasi yake kama chifu wa kijiji hicho sasa iko hatarini

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 05.07.2013 VICHWA VIKUBWA LEO ENEO LA MAZIKO YA MANDELA HADHARANI,CHADEMA YAMNASA LOWWASA,MWIGULU NA MAGUFULI:NINA UTAMANI URAISI.


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.


.
NA MILLAD

EXCLUSIVE PICTURE::HUYU NDO MTOTO WA MSANII IZZO B



Mtoto wa kike wa Izzo B

List ya wasanii wa hip hop Tanzania waliobahatika kupata watoto inazidi kuongeza sasa. Na sasa chama cha wazazi vijana kinamkaribisha rasmi, Emmanuel Simwinga aka Izzo Bizness kundini.Hitmaker huyo wa Love Me, ameshare picha hiyo ya mwanae kwenye Instagram ambaye anaonekana kufanana naye hasa macho, na kuandika ‘Miss Bizness’.
Izzo B  amethibitisha  kuwa huyo ni binti yake na amesema ‘hakuna utajiri mkubwa duniani kama wa mtoto’.
Hongera sana Izzo.

BUNGE LA TANZANIA LAPITISHA KODI YA KADI ZA SIMU (SIM CARD)


Bunge limepitisha sheria ya fedha inayoanzisha kodi kwenye Kadi ya simu. Kila mwenye Kadi ya simu, bila kujali matumizi yake ya simu, atakuwa analipa tshs 1000 kwa mwezi. 

Kodi hii imeanza tarehe 1 Julai 2013. 

Pendekezo hili la kodi lilitolewa na waziri wa Fedha wakati anasoma hotuba yake ya Bajeti. Lakini kwa mshtuko mkubwa nimejua leo kuwa kodi hii iliingizwa kwenye finance bill na kupitishwa. 

Kwa kodi hii maana yake ni kwamba mwananchi wa kawaida, tuseme mwananchi anayefanya kazi ya kuuza maandazi barabarani kila siku, analipa kwa mwezi tshs 1000 sawa sawa na Mbunge ambaye analipwa tshs 11.2m kwa mwezi kama mshahara bila posho za kukaa, posho ya kujikimu na safari mbalimbali. Mwananchi muuza karanga, atalipa sawa na Bakhresa! 

Kinachonishangaza ni kwamba kuna ukimya mkubwa sana kuhusu kodi hii mpya (labda ziara ya Obama). Kodi hii ni mbaya sana. Very rudimentary. Ingawa wabunge wameipitisha, ni vema wananchi wasimame kukataa.