Bunge limepitisha sheria ya fedha inayoanzisha kodi kwenye Kadi ya
simu. Kila mwenye Kadi ya simu, bila kujali matumizi yake ya simu,
atakuwa analipa tshs 1000 kwa mwezi.
Kodi hii imeanza tarehe 1 Julai 2013.
Pendekezo
hili la kodi lilitolewa na waziri wa Fedha wakati anasoma hotuba yake
ya Bajeti. Lakini kwa mshtuko mkubwa nimejua leo kuwa kodi hii
iliingizwa kwenye finance bill na kupitishwa.
Kwa kodi hii maana yake ni kwamba mwananchi wa
kawaida, tuseme mwananchi anayefanya kazi ya kuuza maandazi
barabarani kila siku, analipa kwa mwezi tshs 1000 sawa sawa na Mbunge
ambaye analipwa tshs 11.2m kwa mwezi kama mshahara bila posho za kukaa,
posho ya kujikimu na safari mbalimbali. Mwananchi muuza karanga, atalipa
sawa na Bakhresa!
Kinachonishangaza ni kwamba kuna ukimya mkubwa sana
kuhusu kodi hii mpya (labda ziara ya Obama). Kodi hii ni mbaya sana.
Very rudimentary. Ingawa wabunge wameipitisha, ni vema wananchi wasimame
kukataa.
No comments:
Post a Comment