Majeruhi
wa ajali ya Bajaji Iringa Karim Raphael (14) mkazi wa Mshindo ' A'
katika Manispaa ya Iringa akiwa katika Hospital ya Rufaa ya mkoa
wa Iringa
Majeruhi
wa ajali ya Bajaji Idd Waziri Ng'eng'ena (17) mkazi wa kijiweni
mjini Iringa akiwa na majeraha usoni baada ya ajali hiyo mbaya ya
Bajaji iliyosababisha kifo cha dereva wa Bajaji hiyo
Muuguzi katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa akimpatia matibabu majeruhi Karim
Idd na Karim wakisubiri kupelekwa wodini baada ya kupatiwa matibabu ya awali OPD |
AJALI
mbaya ya Bajaji yasababisha kifo cha dereva wake ambae ni mfanyakazi
wa maduka ya Mzalendo mjini Iringa Bw Sudi Hashimu (22) mkazi wa
Mtwivila huku wengine wawili wakijeruhiwa vibaya.
Ajali
hiyo mbaya imetokea majira ya saa 2 usiku wa kuamkia leo katika
eneo la Mshindo mjini Iringa wakati dereva huyo wa Bajaji akijaribu
kukimbia baada ya kudaiwa kusababisha ajali katika eneo la Miyomboni
mjini Iringa.
Wakizungumza na mtandao wa www.matukiodaima.com majeruhi
wa ajali hiyo Karim Raphael na Idd Waziri Ng’eng’ena walisema kuwa
kabla ya ajali hiyo dereva huyo alikuwa amesababisha ajali kwa
kumgonga mwendesha Bajaji mwenzake na baada ya tukio hilo aliamua
kutimua mbio kwa kutumia usafiri wake wa Bajaji.
Kwani
walisema kufuatia ajali hiyo eneo la Miyomboni ulizuka ugomvi kiasi
cha aliyegongwa kupokonya kofia (Helmenti) ya Bajaji ya Sudi kabla ya
marehemu huyo kufanikiwa kupokonya na kukimbia .
“Katika
Bajaji marehemu alikuwa ametupakia abiria watatu ambapo mmoja aliruka
kabla ya Bajaji hiyo kuchanganya zaidi hivyo tukabaki abiri wawili
na dereva mwenyewe …hata hivyo alionekana kuendesha Bajaji hiyo
kwa sifa zaidi na kuonyesha kuwa yeye ni bingwa wa kukimbiza Bajaji
hiyo” alisema majeruhi Karimu
Hata
hivyo alisema baada ya kufika eneo la Mshindo Kanisani katika tuta
kubwa dereva huyo alishindwa kupunguza mwendo na hivyo kulivaa tuta
hilo wakati akitaka kukata kona na Bajaji hiyo kuacha njia na kugonga
ukuta wa uzio wa Kanisa la RC mshindo na dereva huyo kutanguliza kichwa
katika ukuta huo huku wao wakifunikwa na Bajaji hiyo.
Walisema kuwa dereva huyo alikufa papo hapo huku wao wakishuhudia kifo chake kabla ya wasamaria wema kufika na kuwaokoa.
Kwa
upande wake mmoja kati ya shuhuda wa tukio hilo Mood Mambo
alisema kuwa alifika eneo hilo na kukuta wananchi wakiendelea kutoa
msaada kwa watoto hao ambao walikuwa wamejeruhiwa vibaya na mwili wa
marehemu ukiwa umepasuka kichwa .
Majeruhi
hao walikimbizwa katika Hospital ya rufaa ya mkoa wa Iringa huku
mwili wa marehemu huyu ukihifadhiwa katika chumba cha maiti katika
Hospital hiyo.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)
Ajali
hiyo ni ya pili kusababisha kifo kwa mkoa wa Iringa na ajali ya tatu
mbaya kutokea katika mkoa wa Iringa toka mwaka 2014 ulipoanza ambapo
ajali ya kwanza kusababisha kifo ilitokea wilaya ya Mufindi nay a pili
kujeruhi ilitokea eneo la Ilala wakati wa mkesha wa Mwaka mpya ikiwa ni
dakika 20 kuukaribisha mwaka mpya na kupelekea dereva wa boda boda
kukatwa mguu wake nah ii ni ya tatu .
No comments:
Post a Comment