Msemaji wa jeshi la Uganda Bwana Paddy Ankundal ametangaza kuwa, askari 9 wa nchi hiyo wameuawa na wengine 12 kujeruhiwa katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita nchini Sudan Kusini. Hii ni katika hali ambayo katikati ya mwezi huu Rais Yoweri Museven wa Uganda alitangaza kwamba, askari wa nchi yake wanashiriki katika vita vinavyeendelea nchini Sudan Kusini na kuongeza kuwa, atavumilia hasara yoyote itakayotokana na kadhia hiyo.
Hata hivyo Rais Museven hakuashiria idadi ya wanajeshi wa Uganda waliouawa hadi hivi sasa huko Sudan Kusini. Itakukmbukwa kuwa siku chache tu baada ya kuanza mapigano nchini humo, serikali ya Kampala ilituma askari wake njini Juba kwa madai ya kuwaondoa raia wa Uganda waliokuwa wamekwama nchini humo.
Wiki moja baadaye rais huyo alitangaza kuwa, askari wake wamekuwa wakiwasaidia askari wa serikali ya Rais Salva Kiir katika vita vya kupambana na waasi nchini Sudan Kusini. Kwa mujibu wa ripoti ya siri iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya, siku chache zilizopita Riek Machar makamu wa zamani wa rais wa nchi hiyo, alitangaza kuwa, ndege za Uganda zilijaribu kushambulia eneo alikokuwa amejificha lakini hazikufanikiwa. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Machar anaamini kuwa, kuwepo vikosi vya nchi za nje nchini humo, kunaipunguzia itibari ya jumuiya ya nchi saba za kieneo ya IGAD yenye jukumu la kupatanisha mgogoro huo.
Chanzo, kiswahili.ibir.ir/habari/afrika
No comments:
Post a Comment