Waziri
wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akimsikiliza Baloziwa Norway
(kushoto), Bi. Ingunn Klepsvik pamoja na maafisa wake na kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa DAWASA, Archad Mutalemwa. Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na Balozi wa Norway, Bi. Ingunn Klepsvik.
Balozi wa Norway, Bi. Ingunn Klepsvik, alitembelea Wizara ya Maji na kuonana na Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe.Balozi
huyo alipata fursa ya kuzungumza na Prof. Maghembe kuhusu hali halisi
ya sekta ya maji nchini na miradi mbalimbali ambayo Serikali ya Norway
inafadhili.Bi.
Klepsvik aliambatana na maafisa mbalimbali kutoka ubalozi wa Norway,
huku Wizara ya Maji ikiwakilishwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji,
Inj. Bashir Mrindoko, Kaimu Mkurugenzi wa Maji Mijini, Inj. Amani Mafuru
na Mkurugenzi Mtendaji wa DAWASA, Archad MutalemwaTUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)
No comments:
Post a Comment