Rais Mwenyewe hata hivyo hakujeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea saa mbili asubuhi katika eneo la Limuru eneo la Kati mwa Kenya.
Gari hilo hata hivyo lilipoteza mwelekeo likiwa mbali na msafara wenyewe.Dereva wa gari hilo alipoteza mwelekeo katika barabara kuu ya Nairobi-Limuru.
Waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini.
Rais Kagame alikuwa anarejea mjini Nairobi kutoka katika kongamano la magavana wa Kenya mjini Naivasha katika bonde la ufa .
Kwa sasa Kagame anakutana na Rais Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Rais.
Kagame alialikwa kuhudhuria kongamano la Magavana nchini Kenya kuhusu uongozi mzuri na utawala bora.
Aliwahutubia Magavana hao siku ya Jumatatu na kuwashauri kuwahusisha wananchi katika maamuzi yao ya maendeleo.
Aliwataka kuwahusisha wananchi katika maamuzi ili waweze kujieleza wenyewe kuhusu matatizo na changamoto wanazokabiliwa nazo pamoja na kutafuta suluhisho kwa pamoja.
Mfumo wa serikali za majimbo nchini Kenya ulitokana na katiba mpya ambapo huduma nyingi zilizokuwa zinatolewa na serikali kuu sasa zinapaswa kutolewa na magavana ambao ndio wakuu wa majimbo.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)
Kumekuwa na maandamanao ya mara kwa mara katika majimbo kutokana na magavana kuanza kuwatoza kodi za ajabu wananchi ili kuweza kupata pesa za maendeleo. (BBC)
No comments:
Post a Comment