CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimewasilisha majibu na
pingamizi la awali dhidi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe
kuhusu Kamati Kuu ya Chama hicho akiitaka mahakama kuzuia uanachama wake
usijadiliwe hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa.
Mbali
na majibu hayo na pingamizi la awali, pia chama hicho kimejibu barua ya
Zitto pamoja na kuwasilisha mwenendo wa shauri lililopelekea kuvuliwa
nyadhifa za uongozi katika chama hicho kama mlalamikaji alivyoomba.
Majibu hayo yaliwasilishwa katika Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kupitia
mawakili wa chama hicho, Tundu Lissu na Peter Kibatala ambao
wamewasilisha pingamizi la awali na kutoa hoja sita wakiitaka mahakama
kutupilia mbali kesi hiyo kwa kudai haina mashiko ya kisheria.
Katika
hoja ya kwanza, Chadema kimedai kwamba shauri hilo halina msingi kwa
sababu halikuwasilishwa katika mahakama ya chini kusikilizwa na kutolewa
maamuzi kwa kujibu wa kifungu cha 13 cha Mwenendo wa Mashauri ya Madai.
Hoja
yake ya pili, ni kuwa shauri hilo halina msingi na limewasilishwa
masijala kuu ya Mahakama Kuu badala ya masijala ya Wilaya kinyume cha
sheria na taratibu za masijala za mahakama.
Katika hoja ya tatu, mlalamikaji hajaomba maoni ya Mahakama Kuu kuhusiana na suala linalohusiana na uanchama wake Chadema.
Hati
hiyo inaeleza katika hoja ya nne kwamba shauri hilo halina msingi kwa
sababu Zitto anaendesha mashauri mawili kwa wakati mmoja, Mahakama Kuu
na rufaa ya kwenye Baraza Kuu la chama.
Katika
hoja ya tano, inaleza kwamba shauri hilo Mahakama Kuu siyo mahali pake
kwa sababu Zitto hajatumia nafasi zilizopo ndani ya Chadema.
Hoja
ya sita, Mahakama Kuu haina mamlaka ya kutoa maamuzi ya maombi ya kuzuia
Zitto asijadiliwe uanachama wake kwa sababu ni mambo ya yanayohusu
Chadema.
No comments:
Post a Comment