Katibu
wa CCM Mkoa wa Mjini Mwangi Rajabu Kundya akimnadi mgombea wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Mahmoud Thabit Kombo katika kampeni za uchaguzi mdogo
wa Jimbo la Kiembesamaki zilizofanyika Mbweni Wilaya ya Magharibi
Unguja. (Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar). Mgombea
Uwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi
(CCM) Mahmoud Thabit Kombo akiwahutubia wananchi waliofika katika
kampeni zake Mbweni Wilaya ya Magharibi Unguja.(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).
………………………………………………………………………………………
Na Miza Kona – Maelezo Zanzibar
Chama cha Mapindunduzi ni chama chenye kuleta maendeleo ambacho kinapinga ubaguzi na kuwatetea wananchi haki zao za msingi
Hayo
yameelezwa jana huko Mbweni na Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini Mwangi Rajab
Kundya katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki.
Amesema
kuwa kuna baadhi ya vyama Vya upinzani vinachochea kuleta ubaguzi
nchini kwa kisingizio cha kutaka Zanzibar iwe na mamlaka yake kamili
kinyume na matakwa yao.
Aidha
amesema kuwa Zanzibar imeshapata mamlaka yake tangu baada ya Mapinduzi
na kuundwa kwa chama cha Afro Shirazi Party ASP ambapo tayari ina
viongozi kamili na sifa zake zote za kupata maamlaka hayo.
“Mamlaka kamili tayari yamepatikana tangu ilipoundwa ASP hivyo wanataka mamlaka gani tena”, aliuliza Kundya.
Katibu
huyo ameeleza kuwa Zanzibar itaendelea kudumisha Muungano ambao
unatetea wazanzibar na kuwaletea maendeleo ambayo wananchi wananufaika
na matunda yake.
Amefahamisha kuwa CCM sio chama chenye kuleta ubaguzi kwa wananchi kwani kiko makini katiika kuwaletea maendeleo ya nchi.
Amesema CCM ina viongozi makini ambao ni wataalam wa uongozi hawayumbishwi na watu wasiopenda maendeleo ya nchi.
“Kiongozi
wa watu lazima ajitie katika makundi ya watu ili aweze kujua shida zao
kwa lengo la kutatua matatizo ya watu wao lakini wapinzani hawana
utaala huo”, alifahamisha bwana Kundya.
Aidha
Katibu huyo amewataka wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki kumchagua
kiongozi wa CCM kwani ndiye atakaeweza kusimamia Muungano, kupigania
haki ya wanzibari na maendeleo kwa jumla.
Nae
mgombea uwakilishi wa chama hicho Mahmoud Thabit Kombo ameahidi
kuimarisha matawi ya CCM kwa kinamama na jumuiya za wazazi pamoja na
kuwaimarisha na kuwashajihisha vijana katika mambo ya ajira
No comments:
Post a Comment