· MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI.
· AJALI YA GARI KUACHA NJIA, KUPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO.
· AJALI YA GARI NA PIKIPIKI KUGONGANA HUKO VWAWA MKOANI MBEYA NA KUSABABISHA VIFO.
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI.
MNAMO
TAREHE 29.01.2014 MAJIRA YA SAA 07:30HRS HUKO KAYUTI WILAYANI RUNGWE
TRACTOR LENYE NAMBA ZA USAJILI T.409 BNN LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA
AMASHA SAMSON (28) MKAZI WA KAYUTI LILIGONGANA NA PIKIPIKI YENYE NAMBA
ZA USAJILI T.667 PCE AINA YA BOXER ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA LUSAJO
MWAKAMBA (30) MKAZI WA KYELA NA KISHA KUSABABISHA KIFO KWA ABIRIA WA
PIKIPIKI AITWAYE ALFA MNDENDEMI (24) MKAZI WA MKOANI NJOMBE MUDA MFUPI
WAKATI AKIPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA MAKANDANA – TUKUYU NA
MAJERAHA KWA DEREVA WA PIKIPIKI HIYO . UCHUNGUZI UNAONYESHA CHANZO CHA
AJALI HIYO NI MWENDESHA TRACTOR ALIKATISHA BARABARA GHAFLA KUTOKA
KUSHOTO KWENDA KULIA BILA KUCHUKUA TAHADHALI YOYOTE. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. DEREVA WA TRACTOR AMEKAMATWA. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
AJALI YA GARI KUACHA NJIA, KUPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO.
GARI
LENYE NAMBA ZA USAJILI T.433 ATP AINA YA MITSUBISHI CANTER LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA LILIACHA NJIA KISHA KUPINDUKA
HUKO KATIKA ENEO LA NAMBA ONE WILAYANI RUNGE NA KUSABABISHA KIFO KWA
ANANGISYE STEWAT (27) TINGO NA MKAZI WA IKUTI AKIWA ANAPATIWA MATIBABU
KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. AJALI HIYO ILITOKEA MAJIRAYA SAA
19:30HRS NA UCHUNGUZI UNAONYESHA CHANZO CHAKE NI BAADA YA DEREVA WA GARI
HILO KUPITIWA NA USINGIZI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA
KULITELEKEZA GARI. JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA
KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI. AIDHA ANATOA
WITO KWA WANANCHI/RAIA MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO
HILI AZITOE KWA JESHI LA POLISI ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO
WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
AJALI YA GARI NA PIKIPIKI KUGONGANA HUKO VWAWA MKOANI MBEYA NA KUSABABISHA VIFO.
KATIKA
AJALI NYINGINE GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.784 AVB AINA YA TOYOTA
COASTER MALI YA ILASI SEKONDARI LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA GODFREY
MWALINGO (56) MKAZI WA ICHENJEZYA LILIGONGANA KATIKA ENEO LA ICHENJEZYA
WILAYANI MBOZI NA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.268 CTR AINA YA KING
LION ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA HARUNA JACOB (25) NA KUSABABISHA VIFO KWA
DEREVA HUYO WA PIKIPIKI NA ABIRIA WAKE AITWAYE KELVIN JACOB (21) WOTE
WAKAZI WA ISANGU. AJALI HIYO ILITOKEA MAJIRA YA SAA 07:30HRS ASUBUHI NA
CHANZO CHAKE NI MWENDO KASI WA WA PIKIPIKI, DEREVA AMEKAMATWA. MIILI YA
MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUEPUKA
MWENDO KASI KWANI UNAUA NA NI HATARI.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment