PICHA NA MAKTABA |
Akizungumza na dodoma fm Mwenyekiti wa walemavu bw. Hassan Sharrifu amesema
wanaomba halmashauri kutekeleza agizo la mkuu wa mkoa la kuwapatia viwanja ili waweze kujenga ofisi itakayo wasaidia
kuepukana changamoto zinazo wakabili kutokana na kukosa ofisi.
Aidha bwana
Sharrifu amesema ni vema manispaa ikatambua
shughuli zinazofanywa na chama hicho ili iwape ushirikiano pale panapo
hitajika kwani chama hicho kimekuwa kikijishughulisha na kazi
mbalimbali .
Nae mlemavu wa
ngozi bwana Japheti Andrea amemuomba
Mkuu wa Mkoa kuharakisha zoezi la kuwapatia walemavu maeneo ya kujenga
ofisi hizo ili waweze kuelezea changamoto zinazowakabili
katika chama hicho cha walemavu.
Hayo yamefuatia tamko lililotolewa na mkuu wa Mkoa wa Dodoma bi Rehema Nchimbi ambapo ameitaka
manispaa iwapatie walemavu kutoka kila wilaya eneo kwaajili ya kujenga ofisi.na DODOMA FM
No comments:
Post a Comment