Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa mawasiliano wa Ikulu, Bwana Salva Rweyemamu amesema
kuendeleza mjadala unaohusu mawaziri mizigo ni kupoteza muda, kwani Rais Jakaya Kikwete Alisha maliza kazi yake.
Aidha Bwana Rweyemamu
ameongeza kuwa Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua mawaziri ambao
wanawajibu wa kumsaidia katika utekelezaji wa majukumu yake, hivyo si
sahihi wateule hao kuitwa jina la mawaziri mizigo ikiwa Rais ameona
wanafaa.
Hayo yamejiri mara baada ya Rais Kikwete kuwarejesha katika baraza la mawaziri baadhi ya Mwaziri
ambao walidaiwa kuwa ni mizigo kutokana na udhaifu katika utendaji kazi wao,
baadhi ya mawaziri
hao ni pamaja na Christopher Chiza, waziri wa kilimo chakula na
ushirika,
Dr. Shukuru Kwambwa, waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Hawa Ghasia
na manaibu wake Kasimu Majaliwa, na Agrey Mwanri katika wizara ya nchi,
ofisi ya waziri mkuu (Tamisemi).
No comments:
Post a Comment