Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, January 20, 2014

CHUO CHA ST. JOSEPH TAWI LA SONGEA CHAFUNGWAA BAADA WANACHUO KUGOMA


MKUU WA MKOA RUVUMA atangaza chuo kikuu cha st joseph tawi la songea kufungwa

WANACHUO wa Chuo kikuu cha St,Joseph tawi la Songea waligoma kuingia madarasani na kutoka kufanya shughuli za aina yeyote ndani ya chuo hicho huku wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikwa jumbe mbalimbali zikiwemo zilizoandikwa wamechoka kunyanyaswa na wakufunzi ambao wengi wao raia wa India baada ya uongozi wa serikali ya wanachuo kutimuliwa nyazifa zao na kuwasimamisha masomo kwa muda wa miezi sita.

Kundi la waandishi wa habari wa mjini Songea mara tuu baada ya kupata taarifa ya tukio hilo walifika kwenye eneo la chuo kikuu cha St,Joseph kilichopo eneo la Ruhuwiko mjini Songea ambako walishuhudia maandamano makubwa ya wanafunzi wakiwa wamebeba mabango yaliyo ujumbe mbalimbali ikiwemo ya wamechoka kunyanyashwa na wakufunzi ambao ni wahindi.

Pia wanachuo hao walishuhudiwa wakiimba nyimbo mbalimbali zenye ujumbe wamechoka kunyanyashwa kwani wao ni watu wazima hapaswi kulinganishwa na wanafunzi wa shule za msingi au sekondari huku wimbo mwingine ukiwa na ujumbe kama siyo mwalimu Nyerere kuleta amani wahindi msingefika kwetu kufanya biashara.

Kufuatia mgomo huo ililazimika askari polisi kufika kwenye eneo hilo huku wakiwa wamebeba silaha kwa lengo la kutuliza gasia ambao walitawanywa katika maeneo mbalimbali ya chuo lakini wanachuo waliendelea na maandamano yao huku wakiimba nyimbo za kushinikiza uongozi wa chuo uwarejeshe viongozi wa serikali ya wanachuo kwa sababu ya kutetea haki za wanachuo ambazo walizodai wahidi hao wamekuwa wakizikiuka.
Wanachuo hao ambao walidai kuwa malalamiko yao walishayafikisha kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Saidi Mwambungu wakidai kuwa hali ya mazingira ya chuo hicho siyo manzuri lakini bado wahindi hao wameendelea na vitendo viovu licha ya mkuu wa mkoa kuwaangiza kuwa waache kuunyanyasa uongozi wa serikali ya chuo na wayaweke vizuri mazingira ya chuo hicho ikiwa ni pamoja na kufanyia matengezo ya vyoo ambavyo vimesababisha baad hi ya wanachuo kwenda kujisaidia polini.

Walisema kuwa chuo hicho kinavyoo vyenye matundu na wayaweke vizuri mazingira ya chuo hicho ikiwa ni pamoja na kufanyia matengezo ya vyoo ambavyo vimesababisha baadhi ya wanachuo kwenda kujisaidia polini.

Walisema kuwa chuo hicho kinavyoo vyenye matundu 14 ambapo kati ya matundu hayo saba ya wanawake na saba ni wanaume wakati chuo hicho kinawachuo zaidi ya 1,200 na kufanya kusababisha tundu moja kutumiwa na wanachuo 64 badala ya kati 20 au 25.

Kwa upande wa viongozi wa serikali ya wanachuo waliyotimuliwa Aristides Munjwahuzi na waziri mkuu wake Deogratius Sanga waliwaambia waandishi wa habari kuwa matatizo makubwa yaliyopo ndani ya chuo hicho ni mengi ambayo wanachuo wakijaribu kulalamika kupitia uongozi wa serikali ya wanachuo badala yake uongozi wa chuo umefikia kuufukuza uongozi wa serikali ya chuo na kuwasimamisha masomo kwa muda wa miezi sita jambo lilionekana kuwa ni uonevu mtupu.
Hata hivyo mmoja wa viongozi wa chuo hicho mtawa Antonia Emmanuel alisema kuwa suala la viongozi wa serikali ya wanafunzi la kuvuliwa madaraka na kusimamishwa masomo walishapewa maelekezo kuwa malalamiko yao walete kwa maandishi ili yajadiliwe lakini hawakufanya hivyo jambo ambalo aliliita kuwa ni dharau na badala yake ameshangazwa kuona wanachuo wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali lakini amesema tatizo hilo linahitaji kuwepo mazungumzo ya pande zote mbili yakiwa na lengo la kumaliza tatizo hilo. 
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)

No comments:

Post a Comment