Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, January 20, 2014

PICHA: Mawaziri wapya wala kiapo Ikulu leo


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Jakaya Kikwete akiwa na Makamu wake Dk Ghalib Bilal wakiwa katika picha ya pamoja na mawaziri katika sherehe ya kuapishwa kwa baadhi ya mawaziri wapya iliyofanyika Ikulu jioni ya leo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akiwa na mkewe aliyewahi kuwa Miss Tanzania, Faraja Kotta na  familia yake, baada ya kuapishwa katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Kulia kwa Makamu ni Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba. 
  Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Adam Malima, kuwa Naibu Waziri wa Fedha

  Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Charles Kitwange, kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Amos Makala, kuwa Naibu Waziri wa Maji
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Jenista  Mhagama, kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
  Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Dkt. Pindi Chana, kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Mwigulu Nchemba, kuwa Naibu Waziri wa Fedha
  Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Juma Nkamia, kuwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo
  Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Mahmoud Mgimwa, kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
Wageni waalikwa
Picha kwa hisani ya Ofisi ya Makamu wa Rais

No comments:

Post a Comment