Cristiano Ronaldo amefikisha mabao
400 tangu aanze kucheza soka la kulipwa usiku wa Jumatatu baada ya
kufunga mabao mawili katika mchezo wa ushindi wa 3-0 wa Real Madrid
dhidi ya Celta katika La Liga.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 28, ambaye anapewa nafasi kubwa ya
kutwaa tuzo ya Ballon d'or wiki ijayo, alifunga jumla ya mabao 69 katika
mechi 59 kwa klabu na nchi yake ndani ya mwaka 2013 na mabao yake
mawili ndani ya mwaka huu 2014 yanamaanisha amefikisha jumla ya mabao
400.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United mpaka sasa yupo sawa na
mshambuliaji Pauleta kwa kuongoza kuifungia mabao mengi timu ya taifa ya
Ureno, wote wakiwa wamefunga jumla ya mabao 47, huku akiwa amefunga
mabao 353 kwenye vilabu alivyochezea, hivyo kumpita hata gwiji wa soka
wa Brazil Ronaldo ambaye alifunga jumla ya mabao 352 mpaka alipostaafu
soka.
Mabao 400 ya mshambuliaji huyo mzaliwa wa Madeira yamekuja baada ya
michezo 653, lakini kitu cha kuvutia zaidi mreno akiwa na Real Madrid.
No comments:
Post a Comment