Nyota wa zamani wa Barcelona Ronaldinho amejiunga na klabu ya Besiktas ya nchini Uturuki kwa usajili huru.
Gaucho
mwenye umri wa miaka 33 amesaini mkataba wa miaka 2 na nusu kujiunga na
Besiktas inayoutumia uwanja wa BJK İnönü,taarifa hizi zimedhibitishwa na
gazeti la ‘De Telegraaf‘ la nchini Uholanzi – inasemekana Ronaldinho
atakuwa akilipwa kiasi cha kati ya Euro milioni 10 na 15 kwa mwaka.
Inasemekana
sababu kubwa ya Ronnie kuhamia tena ulaya ni kujaribu kurejesha kiwango
chake ili aweze kumshawishi kocha wa timu ya Taifa ya Brazil Luiz
Felipe Scolari ili aweze kujumuisha jina lake kwenye kikosi cha Brazil
kinachotaraji kushiriki fainali za kombe la dunia baadae mwaka huu.
Hivi
karibuni gazeti la EL PAIS la nchini Uruguay lilimtangaza Gaucho kuwa
mwanasoka bora wa bara la Amerika ya Kusini kwa mwaka 2013 baada ya
kuiongoza timu yake ya Atletico Mineiro kutwaa kombe la Copa
Libertadores kwa mwaka 2013 ikiwa ni pamoja na kufunnga jumla ya mabao
17 na kutoa pasi za mwisho 11 kwenye jumla ya michezo 36 aliyocheza.
No comments:
Post a Comment