Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Peter,
Stephano Kaombe, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa
Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam,
wakati wa harambee ya kuchangia ujnenzi wa Ukumbi huo iliyofanyika leo
asubuhi Jan 26, 2014. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati
alipowasili kwenye Kanisa la Mtakatifu Peter Oysterbay, leo asubuhi kwa
ajili ya kushiriki katika Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Ukumbi wa
mikutano wa Kanisa hilo. ambapo zaidi ya Sh. milioni 65 zilipatikana
kati ya Sh. milioni 600, zinazohitajika hadi ifikapo mwezi Julai. Kati
ya hizo Cash ni Sh. milioni 5 na zilizobakia zikiwa ni ahadi.Picha na
OMR Picha ya pamoja
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Bilal,
akiongoza na na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, kutoka kanisani baada ya
ibada hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza na waumini wa dini ya Kikristu wakati wa Ibada
maalum ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa
la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuhi
Jan 26, 2014. Picha na OMR Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Mwadhama Cardinari Polycap Pengo, wakati wa ibada
maalum ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa
la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuhi
Jan 26, 2014. Picha na OMR
Baadhi ya waumini wa dini ya Kikristu waliohudhuria Ibada hiyo kwenye ibada hiyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Bilal, akiongoza na na
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, kutoka kanisani baada ya ibada hiyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa wakati
alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa
Kanisa la Mtakatifu Peter, baada ya ibada maalum ya harambee ya
kuchangia ujenzi huo, iliyofanyika leo asubuhi, Jan 26, 2014. Kushoto ni
Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Peter, Stephano Kaombe. Picha na OMR
……………………………………………………………………….
Zaidi ya shilingi milioni 65 zimekusanywa
katika harambee iliyoongozwa na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib
Bilal kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa Kanisa la
Mtakatifu Peter lililoko jijini Dar es salaam.
Kati
ya fedha hizo zilizokusanywa katika ibada maalum ya kuchangia ujenzi wa
jengo la ukumbi huo ilyoongozwa na Mhadhama Kadinali Polycap Pengo
kiasi cha shilingi milioni 60.5 zilikuwa ni ahadi na shilingi milioni 5
zikiwa ni fedha taslimu.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Makamu wa Rais aliwahakikishia Watanzania kuwa
serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za taasisi za kidini katika
kudumisha amani na upendo ndani ya jamii bila ya kujali tofauti za aina
yo yote ile.
Alisema
kuwepo kwake katika hafla hiyo ni ishara ya uhusiano mkubwa uliokuwepo
kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taasisi mbali
mbali za dini nchini.
“Sisi
Watanzania tumefika hapa kutokana na uongozi thabiti wa waasisi wa
Taifa letu. Hivyo, tunataka nchi ya watu wanaomwogopa Mungu, watu
wanaopendana, watu wanaovumiliana na watu wanaotakiana mema katika
shughuli zao.”
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Bibi Rose Rupia kamati yake
inahitaji shilingi milioni 600 zaidi kukamilisha hatua za mwisho za
ujenzi wa jengo la ukumbi huo na kwamba tayari wameshatumia kiasi cha
shilingi bilioni moja katika ujenzi huo.
Ibada hiyo maalum ilihudhuriwa pia na viongozi mbali mbali akiwemo Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa.
No comments:
Post a Comment