Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, January 10, 2014

HABARI NJEMA KWA MOYES, RVP AREJEA!!


STRAIKA hatari wa Mabingwa Manchester United, Robin van Persie, amerejea tena kwenye Mazoezi kamili na wenzake hapo Jana huko Carrington baada ya kuwa nje ya Uwanja kwa Mwezi mmoja akiugua maumivu ya Paja.
Ingawa hataweza kucheza Mechi ya Jumamosi hii ya Ligi Kuu England na Swansea City Uwanjani Old Trafford, Van Persie anatarajiwa kuwa fiti kwa ajili ya Mechi ya Ligi ya Jumapili ya Wiki ijayo dhidi ya Chelsea Uwanjani Stamford Bridge.
Hivi Juzi, Van Persie alirejea kutoka kwao Holland alikokuwa kwenye Mazoezi maalum ya Wiki mbili kwa Kocha wa Viungo wa PSV Eindhoven Arno Phillips ambae amewahi kushirikiana nae huko nyuma.
Msimu huu, Van Persie, ambae hushirikiana vyema na Wayne Rooney, amefunga Bao 10katika Mechi 16 na Wadau wote wanaomba ushirikiano huu udumu na kuokoa Msimu wa Man United ambao wameanza ovyo Mwaka 2014 kwa kufungwa Mechi zao zote 3 hadi sasa.
WAKATI HUO HUO, Kocha wa zamani wa Timu ya Vijana ya Man United, Eric Harrison, amedai David Moyes, Meneja wa Man United anaesakamwa na Matokeo mabovu tangu ashike hatamu mwanzoni mwa Msimu, hakupaswa kuliondoa Benchi lote la Ufundi la Sir Alex Ferguson.
Alipotua Man United, Moyes alikuja na Wasaidizi wake kutoka Everton na kumteua Veterani Ryan Giggs kama Kocha Mchezaji.

Harrison ametamka: “Hakika walitakiwa kubakisha Benchi la Ufundi lilelile la Ferguson. Nina hakika Sir Alex ataongea na Moyes lakini hatampa amri: ‘fanya hivi, fanya lile’ bali atamwambia kistaarabu nini kinapaswa kufanywa. Nadhani wawili hawa wanapaswa kukutana mara kwa mara na Moyes kumsikiliza kwa makini Sir Alex!”

No comments:

Post a Comment