………………………………………………………………………………………
Na Immaculate Makilika –Maelezo.
Serikali
ya Jamhuri ya watu wa China jana katika uwanja wa Taifa wa Uhuru
jijini Dar es salaam imesheherekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwa
uhusiano baina ya China na Tanzania ,ikiwa pia ni siku ya mwaka mpya wa
kichina ambayo hujulikana kama sikukuu ya “Spring”.
Katika
kusheherekea siku hiyo Serikali ya China pamoja na makampuni
yamechangia zaidi ya milioni 300 katika huduma za kijamii,huku michango
hiyo ikiwa kama ifuatavyo; Serikali ya watu wa China imechangia milioni
100 kwa ajili ya kuchimba visima,Uhifadhi wa wanyamapori na mafunzo kwa
wenyeji,wafanyabiashara wa China wamechangia milioni 50 kwa ajili ya
visima na elimu huku Jumuiya ya Ujenzi wa Afrika wamechangia milioni 15
kwa ajili ya viatu vya wanafunzi.
Halikadhalika,Kampuni
ya Madawa imechangia milioni 25 kwa ajili ya madawa ya kutibu
malaria,huku milioni 100 zilichangwa na Jumuiya ya Muungano wa Wachina
na fedha hizo zikielekezwa kwa vijana na wananchi wa Tanzania na
kuhitimishwa na mchango kutoka Benki ya Biashara ya China ambayo
imechanga milioni 20 kwa ajili ya vijana na elimu ya Tanzania.
Aidha
,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary
Nagu aliyekuwepo kwenye sherehe hizo kwa niaba ya Waziri Mkuu Mizengo
Pinda, aliwashukuru sana watu Serikali ya China pamoja na
wafanyabiashara na makampuni hayo kwa misaada katika kuchangia
maendeleo ya huduma za kijamii kwa watanzania.Urafiki wetu utaendelea
kukua kwa faida ya watu wetu kama alivyosema waziri Nagu “China na
Tanzania tunaurafiki wa dhati kwa muda mrefu sasa”.
Balozi wa
China nchini Lu Youqing kwa upande wake alisema mwaka huu si tu
kusheherekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lakini pia
ni miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China
na Tanzania.“Mwaka uliopita nchi hizi mbili zilikua na ziara kwa kiasi
kikubwa ,huku tukishuhudia ujio wa Rais wa China Xi jinping, hali hiyo
imeleta msukumo mpya wa mahusiano unaolenga kuleta manufaa yenye usawa
kwa nchi hizi mbili”.
Alisema
watu wa China wamejidhatiti katika kujenga Taifa lao la China, watu wa
Tanzania na Afrika kwa ujumla pia wamejidhatiti kufufua ndoto za
maendeleo kwa nchi zao,tuungane sote pamoja katika kutimiza ndoto zetu
za maendeleo katika mwaka huu mpya.
Sherehe
hizo zilizohudhuriwa na idadi kubwa ya wananchi wa China nchini,huku
wakionekana wenye furaha wakati wote na kufuatilia kwa makini kila aina
ya burudani iliyokuwa ikiendelea uwanjani hapo.
Bwana
Jerome Wu,mwananchi wachina alisema hii ni mara yake ya tatu kuhudhuria
sherehe za mwaka mpya wa kichina akiwa nchini Tanzania na kuongeza kuwa
amefurahishwa sana na utofauti uliopo mwaka huu,na kupongeza jitihada
zinazofanywa na Serikali za nchi hizi mbili katika kudumisha urafiki huo
na kuongeza kuwa yeye hupata fursa ya kukutana na jamaa na marafiki
kwenye sherehe hizi.
Aidha
viongozi mbalimbali wa Serikali na Jeshi walihudhuria ikiwemo Waziri
wa Katiba na Sheria Dr. Asha Rose Migiro,Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka na Naibu Waziri wa Nishati na
Madini Stephen Masele.
Uhusianao
baina ya nchi hizi mbili ulianzishwa na Baba wa Taifa hayati Mwl Julius
Nyerere na Mwenyekiti Mao Zedong kwa nia ya kuhudumia wananchi
wao,hatahivyo umekua ni uhusiano wenye manufaa makubwa kwa kusaidia
kujengwa kwa reli ya Tanzania – Zambia,kiwanda cha nguo Urafiki, uwanja
wa Taifa Uhuru, na miradi mingine ikiendelea ikiwa ni pamoja na ujenzi
wa Bandari ya Bagamoyo na bomba la gesi asilia toka Mtwara wakati miradi
hiyo ikitazamiwa kuboresha uchumi na maisha ya watanzania pamoja na
kudumisha urafiki huu baina ya Tanzania na China.
No comments:
Post a Comment