JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LAFANIKIWA KULIPATA GARI LILILOPORWA KATIKA TUKIO LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA.
· WATU WANNE WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA KIKONGWE.
· WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI.
· WATU WAWILI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLIS KWA KUKUTW A NA BHANGI
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LAFANIKIWA KULIPATA GARI LILILOPORWA NA WATU
WANAODHANIWA KUWA NI MAJAMBAZI KATIKA TUKIO LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA
SILAHA. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 25.01.2014 MAJIRA YA 20:00HRS
HUKO MAENEO YA ISYESYE JIJINI MBEYA AMBAPO OBADIA JONAS {41}
MFANYABIASHARA NA MKAZI WA ISYESYE ALINYANGANYWA GARI LAKE LENYE NAMBA
ZA USAJILI T.675 CLX AINA YA TOYATA KLUGER. MUHANGA ALIVAMIWA NA KUNDI
LA WATU WASIOFAHAMIKA AKIWA GETINI KWAKE AKITOKEA KATIKA BIASHARA ZAKE
MAENEO YA ILOMBA JIJINI MBEYA, WATU HAO WAKIWA NA SILAHA AINA YA SMG
PAMOJA NA MAPANGA WALIPIGA RISASI MBILI HEWANI KISHA KUWAAMURU KUSHUKA
NDANI YA GARI NA KUMJERUHI MUHANGA KATIKA PAJA LA KULIA NA BAADAE
KUONDOKA NA GARI HILO PAMOJA NA PESA TASLIM AMBAZO THAMANI YAKE BADO
KUFAHAMIKA. JESHI LA POLISI LILIFANYA JITIHADA ZA MARA MOJA NA
KUFANIKIWA KULIPATA GARI HILO. MSAKO MKALI UNAENDELEA KUWASAKA
WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI. MAJERUHI AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA KWA MATIBABU. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHANA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII/WANANCHI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA WALIKO WATUHUMIWA HAO
AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAO. PIA AMEWATAKA WAFANYABIASHARA WAWE MAKINI KATIKA
KUSAFIRISHA FEDHA TOKA ENEO MOJA KWENDA LINGINE NA NI VYEMA WAWE NA
USIRI.
WATU WANNE WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA KIKONGWE.
|
JESHI
LA POLISI MKOA HAPA LINAWASHIKILIAWATU WANNE KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA
MAUAJI. TUKIO LILITOKEA HUKO KATIKA KIJIJI CHA KALOBE KATA YA KIMO
TARAFA YA UKUKWE WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. AMBAPO EDNA KAJINGA
{70} MKAZI WA KATOBE ALIFARIKI DUNIA TAREHE 25.01.2014 KATIKA HOSPITALI
YA RUFAA MBEYA WAKATI AKIPATIWA MATIBABU BAADA YA KUVAMIWA USIKU WA
TAREHE 22/01/2014 MAJIRA YA SAA 03:30HRS NA KUPINGWA RUNGU KICHWANI NA
MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA KUWA CHANZO CHA
MAUAJI HAYO NI IMANI ZA KISHIRIKINA. WATUHUMIWA WANNE [04] WANASHIKILIWA
NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA KATIKA TUKIO HILO, MAJINA YAO
YANAHIFADHIWA KWA SABABU ZA KIUPELELEZI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMEDI Z. MSANGI ANATOA
WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA MAUAJI YA KWA IMANI ZA KISHIRIKIA KWANI
NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANAOMBA USHIRIKIANO TOKA KWA WANANCHI
KATIKA KUWABAINI/KUWAFICHUA WALE WOTE WENYE TABIA ZA AINA HII KWANI
WANAISHI KATIKA JAMII HIZO NA BILA KUWEPO USHIRIKIANO JUHUDI ZA KUMALIZA
UHALIFU WA AINA HII HAUTAFANIKIWA SANA.
WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI.
MNAMO
TAREHE 25.01.2014 MAJIRA YA SAA 19:30HRS HUKO KATA YA CHIMBUYA TARAFA
YA IYULA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA WATU
WAWILI WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA DAUDI ABEL MKAZI WA S/WANGA {43} NA
CHRISTINA JOSEPH {43}, MKAZI WA S/WANGA WALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO NA
WATU WENGINE WATATU KUJERUHIWA AMBAO NI 1.MICHAEL BUKUKU, 2. JOSIA
MWASANYAPALE, NA 3. ENOS DANIEL, BAADA YA GARI NO. T.978 BSK AINA YA
TOYOTA PRADO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA DAUDI ABEL @ MWAMBAO{43}
MKAZI WA SUMBAWANGA LIKITOKEA S/WANGA KWENDA MBEYA KUGONGANA NA GARI NO.
T.692 AWC MITSUBISHI FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA MICHAEL BUKUKU
{21} MKAZI WA MPEMBA LIKITOKEA VWAWA KWENDA TUNDUMA. UCHUNGUZI WA AWALI
UNAONYESHA CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA MAGARI YOTE MAWILI.
MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA VWAWA NA MAJERUHI
WAMELAZWA HOSPITALINI HAPO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMEDI Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA
KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA
AJALI/MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
WATU WAWILI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLIS KWA KUKUTWA NA BHANGI.
JESHI
LA POLISI MKOA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KOSA LA KUPATIKANA
NA BHANGI KUPITIA MSAKO ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA MNAMO
TAREHE 25.01.2014 MAJIRA YA SAA 06:30HRS HUKO ENEO LA MLOWO JUMA
MWASHIUYA {28} NA BARTON SHITINDI {29} WOTE WAKAZI WA MAJENGO MLOWO
WALIKAMATWA WAKIWA BHANGI HIYO YENYE UZITO WA KILO GRAMU 3. TARATIBU ZA
KISHERIA ZINAFANYIKA ILI KUWAFIKISHA MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHANA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA
WITO KWA VIJANA/JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA NA HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA MBEYA.
No comments:
Post a Comment