Askari wakichukua moja ya miili ya waliofariki katika ajali hiyo eneo la tukio. |
Mtoto
wa miezi sita aliyejeruhiwa kwenye ajali ya gari dogo la abiria la
Toyota Noah na lori la Scania mkoani hapa juzi, amefariki dunia na
kufanya idadi ya waliokufa kufikia 14.
Happiness Elisha alifariki dunia jana akiwa katika Hospitali ya St Gaspar, Itigi alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa, Geofrey Kamwela alisema jana, kwamba mtoto huyo na
mama yake, Regina Masalu (27) baada ya ajali hiyo, walikimbizwa katika
hospitali hiyo na wasamaria waliofika eneo la tukio mapema.
Alisema
Regina na mwanawe ni wakazi wa Nkalankala wilayani Mkalama mkoani hapa
na kwamba mama huyo anaendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo, na
hali yake inaelezwa kuwa mbaya.
Aidha,
Kamanda Kamwela alisema miili ya watu watatu ambao walikuwa
hawajatambuliwa, tayari imetambuliwa kuwa ni ya Martin Marko (30) mkazi
wa Itigi, Daniel Emmanuel (24) na Swalehe Hamisi (28) wote wakazi wa
Saranda, Itigi.
Kamwela
alisema abiria waliokuwa kwenye Noah, walikuwa 16 na si 14, kwa kuwa
kuna majeruhi kwenye hospitali ya mkoa, ambaye anaendelea vizuri na
mwingine yuko Hospitali ya Itigi.
Siku
ya ajali, Noah ilikuwa ikitoka Itigi kuja mjini hapa, ndipo iligongana
uso kwa uso na lori ambalo lilikuwa likitoka Mwanza kwenda Dar es Salaam
eneo la Isuna, barabara kuu ya Singida–Dodoma. Watu 13 waliokuwa kwenye
Noah, walipoteza maisha papo hapo.
No comments:
Post a Comment