Elisante
Saidi (51) mkazi wa kijiji cha Nduamughangawilaya ya Singida, akiwa
amelazwa katika hospitali ya mkoa mjini Singida,baada ya kukatwa katwa
Mapanga na kuchomwa Mkuki wa watu wanaodaiwa ni wakazi wa kijiji cha
Handa wilaya ya Nchemba mkoa wa Dodoma.Wakazi hao wa Nduamughanga,
inadaiwa walikuwa wanataka kuwakomboa Ng’ombe wao zaidi ya mia moja
waliokamatwa baada ya kuingia kinyume na sheria kwenye pori la akiba la
Mgori.
Nesi
wa wodi namba tatu katika hospitali ya mkoa mjini Singida, Elionora
Matayi akieleza juu ya kumpokea majeruhi Elisante Saidi aliyenusurika
kuuawa na wakazi wa kijiji cha Handa wilaya ya Nchemba mkoa wa
Dodoma,ambao walikuwa wanataka kuwakomboa kwa nguvu Ng’ombe wao zaidi ya
mia moja waliokamatwa baada ya kuingia kwenye hifadhi ya pori la
Mgori.(Picha na Nathaniel Limu).
Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida,SACP,Geofrey Kamwela, akitoa taarifa kwa
waandishi wa habari iliyohusu mhudumu wa wanyapori kijiji cha
Nduamughanga wilaya ya Singida, kuuawa kwa kukakatwa mapanga kwenye
ugomvi wa kugombea Ng’ombe zaidi ya mia moja.Ng’ombe hao mali ya wakazi
wa kijiji cha Handa wilaya ya Nchemba mkoa wa Dodoma,walikamatwa baada
ya kuingia kwenye hifadhi ya msitu wa Mgori.
.Ni baada ya mifugo kukamatwa kwa kosa la kuvamia hifadhi.
.Watumia nguvu kuvamia hifadhi ili kuchukua mifugo yao kibabe
Na Nathaniel Limu, Singida
WATU
wasiojulikana idadi yao wakazi wa kijiji cha Handa wilaya ya Nchemba
Mkoani Dodoma, wamemuua mhudumu wa wanyamapori, Athumani Jumanne (40)
kutoka cha kijiji cha Nduamughanga kwa kumkatakata mapanga sehemu zake
mbalimbali za mwili.
Kifo cha Athumani inadaiwa kinatokanana kukatwa katwa mapanga kichwani na kupigwa mshale mdomoni.
Inadaiwa
kuwa mauaji hayo yanatokana na ugomvi wa kugombea ng’ombe 180 wa wakazi
wa kijiji cha Handa wilaya ya Nchemba mkoani Dodoma.
Inasemekana walikamatwa na mhudumu wa wanyamapori baada ya kuingia isivyo halali kwenye hifadhi ya akiba yam situ wa Mgori.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Singida, Geodfrey Kamwela amesema kuwa Athumani
ameuawa januari 21 mwaka huu saa saba na nusu huko katika kijiji cha
Nduamughanga kata ya Mughanga tarafa ya Mgori wilaya ya Singida.
Amesema
siku ya tukio,kundi kubwa la wakazi wa kijiji cha Handa,waliingia
katika kijiji cha Nduamughanga wakisaka kuwakomboa ng’ombe wao 180
waliokamatwa kwa kosa la kuingia ndani ya akiba ya hifadhi ya msitu wa
Magori.
Akifafanua,Kamwela
amesema uchunguzi wa awali unaonyesha wazi kuwa chanzo cha mauaji hayo
ni ugomvi wa kugombea ng’ombe hao 180 waliokamatwa baada ya kuingia
kwenye hifadhi ya akiba ya pori la Mgori.
“Wengi
wa watu hao wamewahi kuvamia na kuishi katika eneo la akiba ya hifadhi
ya msitu wa Mgori.Kutokana na kuishi kwa muda mrefu kwenye eneo hilo na
baadaye kutolewa kwa nguvu,walikuja wakiwa na orodha ya majina ya watu
ambao walitarajia kuwauawa”,amesema.
Kamanda
huyo amesema kuwa baada ya kuvamia kijiji hicho cha
Nduamughanga,waliweza kuwajeruhi Hamisi Ramadhani (36),Elisante Saidi
(51),Omari Omari (42),Muna Hamisi (38) na afisa mtendaji wa kijiji cha
Nduamughanga Mwaftari Rajabu (35).
Alitaja
wengine kuwa ni Abrahamu Mhamed(60),Hnis Rajabu (33),Yohana Saidi
(37),Ramadhani Rajabu (26),Msafiri Juma,Omari Hamisi (33),Hamisi Sharifu
(32),Jumanne Hasani ,Abdi Musa,Daudi Karata,Helena Bakari (65) na
Jumanne Musa (28).
“Majeruhi
hao wote isipokuwa Elisante Said,waliweza kupatiwa matibabu katika
zahanati ya kijiji cha Nduamughanga na kuruhusiwa kuondoka.Elisante yeye
amehamishiwa katika hospitali ya mkoa iliyopo mjini hapa,na bado
anaendelea na matibabu kutokana na kuumizwa vibaya”,amesema kamanda
huyo.
Amesema
kundi hilo baada ya kujeruhi watu hao 17,waliweza kumsaka mhudumu wa
wanyamapori Athumani na walipompata,walimkata kata mapanga kichwani na
kumpiga mshale mdomoni na kusababisha kifo chake papo hapo.
Kamanda Kamwela amesema kuwa baada ya hapo,walianza kusaka mahali ng’ombe wao wamehifadhiwa ili waweze kuwachukua kwa nguvu.
“Hawakuweza
kuwapata ng’ombe wao 180 na badala yake walipora ng’ombe 68,mbuzi
101,kondoo sita na punda watatu mali ya Abrahamani Mohammed (60)
waliokuwa wakichungwa mbugani,na kuondoka nao”,amesema Kamwela.
Amesema
hadi sasa wamefanikiwa kuwakamata Nicodemo Ako (45) mkazi wa kijiji cha
Giting wlaya ya Hanang mkoa wa Manyara na Athumani Soa (62) mkulima na
mkazi wa kijiji cha Handa.Baada ya kumaliza uchunguzi,watu hao wawili
watafikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment