Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Deo Filikunjombe alisema kuwa wanatarajia
kupokea taarifa hiyo ili kujihakikishia kama matumizi hayo yalikuwapo au kulikuwa na ulaghai wa aina yoyote.
Aidha amesema Kwa sasa ni mapema kuanza kufikiri kwamba fedha
hizo hazikutumika kama inavyotakiwa, lakini kama kuna ujanja
wowote ulifanyika utabainika ndio maana wametaka kukutana na wizara ya
Fedha( CAG)pamoja na Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi ili kupata
majibu ya
papo kwa papo.
Novemba mwaka jana Serikali ilianza kusambaza vitabu milioni
19.4 kwa shule za msingi nchini, ambavyo ilielezwa kuwa vimenunuliwa kwa
chenji
ya rada na asilimia 75 ya fedha hizo zimetumika kununulia vitabu hivyo
na asilimia 25 zitatumika kununulia madawati.
No comments:
Post a Comment