Akizungumza na kituo hiki afisa elimu wa wilaya ya chamwino
bi. Scola Kapinga amesema changamoto kubwa inayo ikabili wilaya ya
chamwino katika Secta ya Elimu ni upungufu wa madawati hususani katika
shule za sekondari.
Aidha Bi Kapinga ameongeza kuwa mwaka jana walikuwa na
kampeni ya kuwahamasisha wazazi kutengeneza madawati kwaajili ya
matumizi ya wanafunzi.
Sanjari na hayo bi Kapinga amesema kuna baadhi ya vijiji
katika wilaya hiyo vimeanza kuweka mpango wa kutengeneza dawati
moja kwa kilakaya ambapo mpango huo utarajia kuanza ifikapo mwezi
octoba mwaka huu.
WAKAZI MKOANI HAPA WAMEPATIWA MSAADA WA CHAKULA KUTOKA NA UPUNGUFU WA CHAKULA ULIO YAKUMBA BAADHI YA MAENEO.
Akizungumza na Dodoma fm Afisa Kilimo wa mkoa wa Dodoma Bwana
Benard Abraham amesema Mkoa wa Dodoma ulipata tani 1672.3 ambapo tani
167.1 ni ya chakula kinacho tolewa bure na tani 1505.2 ni ya chakula
kitakacho nunuliwa kwa bei nafuu.
Aidha Bwana Abraham amezitaja wilaya zilizonufaika na msaada
huo wa chakula kuwa ni pamoja na wilaya ya Mpwapwa, Dodoma
mjini , wilaya ya Kongwa, Chamwino pamoja na wilaya ya Bahi.chanzo DODOMA FM
No comments:
Post a Comment