Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, January 30, 2014

KAMATI YA PAC YAFANYA UKAGUZI VITABU VYA CHENJI YA RADA DAR

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, (CHADEMA), Zitto Kabwe, akiwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam Jumatano Januari 29, 2014, akikagua vitabu vya ziada. Kamati ya bunge ya PAC, ilifanya ziara ya kushtukiza shuleni hapo ili kubaini kama vitabu vilivyonunuliwa kutokana na chenji ya rada vimekwishagawiwa kwenye shule mbalimbali kama ilivyoahidi serikali. Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, kamati yake ilikuta vitabu hivyo vikitumiwa na wanafunzi.

Zitto akizungumza na wanafunzi
Wanafunzi wakipiga makofi, wakati mwenyekiti huyo akizungumza nao
Wanafunzi wakisikiliza maelezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC), ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, kwenye shule ya msingi Bunge katikati ya jiji la Dar es Salaam Jumatano Januari 29, 2014.Picha na K-Vis Blog

No comments:

Post a Comment