Mkurugenzi
Mtendaji wa Huduma za Kipolisi wa Interpol Bw. Jean-michel Louboutin
kushoto akimkabidhi Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamdam Omari Makame
nembo maalum ya Interpool,
…………………………………………………..
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
SHIRIKISHO
la Polisi wa Kimataifa Duniani INTERPOL, limesema litaendelea kuunga
mkono juhudi zozote zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika
kuboresha na kudumisha hali ya usalama wa Visiwa vya Zanzibar kwa lengo
la kuimarisha utalii kwenye eneo hilo.
Ahadi
hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma za Kipolisi wa
Interpol Bw. Jean-michel Louboutin, wakati alipokutana na Kamishna wa
Polisi Zanzibar CP Hamdani Omari Makame, aliyetembelea Makao Makuu ya
Shirikisho hilo mjini Lyon Ufaransa ambapo walijadili mambo mbalimbali
ya kiusalama yanayoigusa Zanzibar kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.
Bw.
Jean-michel amesema ipo haja kwa jumuia nyingine za kimataifa kuunga
mkono juhudi za Tanzania katika suala zima la kuimarisha usalama wa eneo
hilo lenye historia inayovuta watalii kutoka katika mataifa mbalimbali.
Katika
ziara hiyo ambayo ililenga kuimarisha usalama wa kikanda, Kamishna
Hamdani alisema kuwa Jeshi la Polisi nchini Tanzania litaendelea kutoa
msukumo na kushirikiana na Interpol ili kusaidia katika mapambano ya
uhalifu wa kimataifa.
Kamishna
Handani ameutaja uhalifu ambao ni kero na kikwazocha uchumi kuwa ni
pamoja na Ugaidi, Uharamia, Biashara haramu ya dawa za kulevya na
uhalifu mwingine unaovuka mipaka.
Kamishna
Hamdani ambaye amekabidhiwa nembo maalum ya Interol, pia alipata fursa
ya kutembelea vitengo mbalimbali vya Makao makuu ya Interpol na kupatiwa
muhtasari wa mafunzo yanayotolewa na Interol katika kuwajengea uwezo wa
kiutendaji Maafisa na Askari wa kada mbalimbali.
No comments:
Post a Comment