KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Hamis
Kiiza amesema kuwa aliyekuwa kocha wao mkuu, Ernest Brandts amejitakia
kufukuzwa kwenye timu hiyo inayojiandaa na Ligi Kuu Bara na michuano ya
kimataifa.
Hiyo ni siku chache tangu uongozi wa
timu hiyo kutangaza kulitimua benchi zima la ufundi lililokuwa
linaongozwa na kocha huyo na msaidizi wake Fred Minziro na kocha wa
makipa Mkenya, Razack Siwa kwa kilichodaiwa kushindwa kazi na kuzidiwa
uwezo na kikosi hicho.
Akizungumza na Mwanaspoti, Kiiza alisema
kuwa siku zote Yanga wanataka matokeo mazuri ya ushindi na si kingine,
hivyo kocha huyo alikuwa akipanga timu kwa mazoea.
"Ujue kocha wetu (Brandts) amejitakia
mwenyewe kufukuzwa kwenye timu, ameshindwa kujua Wanayanga wanataka
nini, wao wanataka matokeo mazuri ya ushindi si kingine.
"Ninaamini kama timu ingekuwa inapata
matokeo katika mechi zake, basi angeendelea kubaki kuifundisha Yanga, si
kocha mbaya ni mzuri tena ana uwezo mkubwa wa kufundisha, lakini hilo
la matokeo ndiyo limemwondoa.
"Hakuwa makini katika kupanga timu
itakayopata matokeo mazuri kwenye mechi, alikuwa akipanga timu kutokana
na mazoea. Aliogopa baadhi ya wachezaji kwa kuwapanga kikosi cha kwanza
katika mechi wakati uwezo wao ni mdogo,'' alisisitiza mchezaji huyo bila
kutaja majina ya wachezaji ambao uwezo wao mdogo.
Kiiza ambaye pia aliwahi kutofautiana
waziwazi na Brandts aliongeza: "Mashabiki wa Yanga wanataka matokeo
mazuri, sichagui kocha wa kufanya kazi naye, yeyote yule nitampa
ushirikiano
No comments:
Post a Comment