picha na maktaba |
Na Mwinyi Sadallah, Mwananchi
Zanzibar.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana amesema ameamua kuweka kambi
Zanzibar, lengo likiwa ni kuimarisha chama hicho na kuhakikisha CCM
inarejesha majimbo yake yaliyopotea tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama
vingi mwaka 1995.
Kinana
aliweka msimamo huo kwenye mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa miaka 37 ya
kuzaliwa CCM, uliofanyika uwanja wa Soka Kiembesamaki mjini hapa juzi.
Alisema
kambi hiyo itaanza kabla ya Aprili mwaka huu, kwa kufanya ziara kuanzia
ngazi ya wadi, jimbo, wilaya hadi mikoa kukagua hali ya kisiasa na
kuweka mikakati mipya ya chama hicho kisiwani Zanzibar.
"Nitaanza
ziara maalumu kabla ya sherehe za Muungano, mengi nitayazungumza wakati
huo ukifika, lengo kubwa ni kuangalia uhai wa chama chetu na kuweka
mikakati ya kisiasa kabla ya mwaka," alisema Kinana.
Alisema
kazi kubwa ya CCM ni kutekekeza sera na ilani yake ya uchaguzi tofauti
na vyama vya upinzani, ambavyo ni mahiri na hodari wa kusema bila ya
kuonyesha vitendo.
Katibu
Mkuu huyo aliviponda vya upinzani nchini na kwamba, CCM imewaachia kazi
ya kusema, yenyewe imekijikita kuwatumia wananchi na kutekeleza majukumu
yake ya kisera, mipango na mwongozo.
Kuhusu
Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, Kinana alisema watu waliobeza
Mapinduzi hayo hivi sasa wamefedheheka kwa kushuhudia yakitimiza miaka
50 huku taifa likiwana hali ya amani, umoja na mshikamano.
"Waliodhani
Mapinduzi yatashindwa wameshindwa wao.Tumejiimarisha kwa ulinzi na
usalama, tumejenga umoja, upendo na maelewano, kubwa tukijivunia hatua
za maendeleo yaliofikiwa, " alisema Kinana.
Tangu
kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 na kufuatiwa na uchaguzi
mkuu wa kwanza mwaka 1995, CCM ilipata pigo kubwa kwa kupoteza viti
vyote majimbo Pemba na wakati ikitafakari hayo, CCM ikaendelea tena
kupoteza viti vyake vya Magogoni, Mtoni na Nungwi kisiwani Unguja mwaka
2010.
Viongozi
waliohudhuria mkutano huo wa uzinduzi wa miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,
ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa
Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakili
(BLW), Pandu Ameir Kificho na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai
Ali Vuai.
Wakati
maadhimisho hayo yakifanyika mjini hapa, uchaguzi mdogo wa uwakilishi
Jimbo la Kiembesamaki unatarajiwa kufanyika Jumapili hii.
Uchaguzi
huo unafanyika kufuatia CCM kumfukuza uanchama, aliyekuwa mwakilishi wa
jimbo hilo, Mansoor Yusuf Himid kwa tuhuma za kwenda kinyume na mlengo
wa chama hicho. Alikuwa akipigania kurejeshwa kwa Serikali ya Zanzibar
yenye mamlaka. Baba yake ni miongoni mwa waasisi wa Mapinduzi
No comments:
Post a Comment