Joseph
Konyi kiongozi wa kundi la waasi wa Lord's Resistance Army (LRA) la
nchini Uganda, ameiandikia ujumbe serikali serikali ya nchi hiyo akiomba
msamaha na maelewano ya amani kwa ajili ya kumaliza uasi nchini.
“Nataka
kuwafahamisha watu wa Uganda kwamba, sisi wanachama wa kundi la (LRA)
tumeungana pamoja kwa ajili ya kurejesha amani iliyokumbwa na vita vya
muda mrefu na serikali ya Rais Museven.” Umesema ujumbe wa Kony. Kony
ameongeza kama ninavyo nukuu:
“Tupo
tayari kwa ajili ya kuomba msamaha na kusamehi na pi kudumisha amani na
kumaliza vita hivi vilivyoathiri nchi za eneo la Maziwa Makuu za
Afrika.”
Mwisho wa
kunukuu. Mazungumzo kati ya serikali ya Unganda na kundi la waasi wa
Lord's Resistance Army (LRA), yaliyokuwa yakiendelea mjini Juba, Sudan
Kusini, yalikwama baada ya Joseph Konyi kukataa kutia saini makubaliano
ya mwisho mwaka 2008.
Joseph Konyi kiongozi wa kundi hilo la waasi wa (LRA) anaaminika kujificha nchini Kongo DRC na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
No comments:
Post a Comment