TAMKO LA JUMUIYA YA VIJANA KUUNGA MKONO KAZI YA
SEKRETARIETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI CHINI YA KATIBU MKUU NDUGU
ABDULRAHAMAN KINANA
“..Chama Cha Siasa chochote duniani hubomoka kutokana na migongano
iliyokithiri ya muda mrefu. Uzoefu wa vyama vikubwa vilivyoporomoka
umeonyesha hivyo! Chama lazima kidhibiti uchu wa madaraka wa baadhi ya
viongozi wake na ndani ya serikali yake...” – Dr Eginald P. Mihanjo
“..Chama cha siasa ni itikadi. Chama cha siasa ni siasa kwa maana
halisi ya neno lenyewe siasa –“siasa”. Ni mahali ambapo watu wenye
madhumuni mamoja yaliyoainishwa waziwazi hukutana na
kuwa kitu kimoja.
Chama cha siasa sio mkusanyiko wa “majini dume yenye tamaa”, - majini
ambayo yametanguliza mbele tamaa kufa na kupona-tamaa ya kutengeneza
pesa au kupata vyeo kwa gharama yoyote! – Dr Bashir Ally
UTANGULIZI:
Hili ni tamko la vijana makini wa jumuiya ya umoja wa vijana wa Chama
Cha Mapinduzi (UVCCM) kuunga mkono juhudi na utendaji wa sekretarieti
ya halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi ikiongozwa na Katibu Mkuu
Komredi Abdulrahaman Kinana.
Maneno ya utangulizi yamebeba dhima ya tamko hili, kufuatia taarifa
zilizoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari vikiwanukuu baadhi ya
wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, wakiwatuhumu Viongozi wa
Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM, Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahaman
Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Moses Nnauye.
Sisi Vijana tunatambua kuwa tuhuma hizo na maneno hayo ya hovyo
yametolewa kwa nia ovu yenye kulenga kuwakatisha tamaa Viongozi hao wa
Chama. Tunafahamu kuwa upo mkakati wa kiuhaini ulioandaliwa na
kuratibiwa na “mtandao” ndani ya Chama ambao umejipanga kuendesha
uhaini huo.
Sisi vijana wa UVCCM tunatambua na kuthamini juhudi za Katibu Mkuu na
Sekretarieti yake katika kukijenga na kukiimarisha Chama kwa
kuisimamia barabara misingi na shabaha ya kuundwa kwake, katika umri
wetu hatukuwahi kuona Chama kikiwa karibu na wananchi kwa kufuatilia,
kusikiliza na kushiriki katika utatuzi wa kero, shida na changamoto
zao kama ilivyo katika kipindi hiki chini ya Comrade Kinana na timu
yake. Juhudi hizi ni za kuungwa mkono na kamwe si za kubezwa na
mwanaCCM muadilifu, muaminifu na mwenye mapenzi ya kweli kwa Chama.
Juhudi za kukiimarisha Chama kutoka ngazi za chini, kwa mabalozi ni
mkakati bora kuwahi kutekelezwa na Chama, kukirudisha Chama kwa
wanachama ni kutimiza lengo la kuundwa kwa Chama hiki, Chama hiki ni
cha wanyonge, masikini wa Taifa hili, HAIWEZEKANI matajiri watake
kukihodhi na waratibu mikakati ya kukihujumu kwa pesa zao hali sisi
vijana tukitazama, tunasema tutakilinda Chama chetu na tutawalinda
viongozi wetu waadilifu.
Ni hawa ambao wanabezwa leo ndio wameweza kurudisha Imani ya wananchi
kwa Chama, Imani na matumaini ambayo tayari yalishaanza kupotea na
Chama kuonekana si tena cha wanyonge, wakulima na wafanyakazi wan chi
hii.
Ni Comrade Kinana na timu yake ndio waliozunguka kwenda kukutana na
wakulima wa Pamba kule mikoa ya Kanda ya ziwa na kumpeleka balozi wa
China na kumshawishi kujenga viwanda ili kuboresha manufaa kwa wakulima.
Ni Comrade Kinana na timu yake ndio waliokwenda Kusini kukutana na
wakulima wa Korosho na kushirikiana nao pamoja na bodi kutatua tatizo la
Korosho.
Ni Comrade Kinana na timu yake ndio walioibua hoja na kero za
wafugaji, walimu na wananchi kwa ujumla, na kuwataka viongozi wa
Serikali kuhakikisha wanawajibika kwa wananchi walipa kodi wa Taifa
hili.
Kupinga mafanikio ya Ziara hizo ni kupinga utetezi wa wanyonge.
Mtu anayebeza ziara hizo na kuwaita Viongozi waliozifanya waropokaji na
wahuni wahuni ni mtu mjinga, mtu wa hovyo,hana maadili, asiyekipenda
Chama, mhaini na mzandiki anayepaswa kuchukuliwa hatua kali za
kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine.
TAMKO hili limezingatia wosia wa Baba wa Taifa, muasisi wa Chama Cha
Mapinduzi Mwl Julius Kambarage Nyerere katika kitabu Chake
TUJISAHIHISHE.
“Inapofikia wasimamizi wa Kanuni za Chama wanapigwa vita ya wazi kwa
uamuzi wao wa kukisimamia Chama, tafsir yake ni moja tu watu
wanaowapiga vita hawakitakii mema chama chetu.”
Imetolewa na Paul Christian Makonda.
Katibu wa Hamasa na Chipukizi.
MWENYEKITI WA CCM DKT. SAMIA AONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU CCM TAIFA
DODOMA
-
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 17 Januari 2025, ameongoza
Kikao c...
12 hours ago
No comments:
Post a Comment