Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, January 4, 2014

KUAHIRISHWA KWA SAFARI YA TRENI YA ABIRIA KWENDA BARA HADI JUMAPILI JANUARI 05, 2014


KAMPUNI YA RELI TANZANIA
TAARIFA  KWA VYOMBO VYA HABARI YA  KUAHIRISHA SAFARI YA TRENI YA
ABIRIA KWENDA BARA HADI JUMAPILI JANUARI 05, 2014
  
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawatangazia abiria wote na wananchi kwa jumla  kuwa kutokana na sababu za kiufundi unasikitika kuwa treni ya abiria iliyopangwa kuondoka jana  Ijumaa Januari 03, 2014 saa 3 usiku  imeahirishwa  hadi  kesho Jumapili Januari 05  Machi 16, 2013, saa 3 usiku.
Taarifa imefafanua kuwa kutokana na mvua kunyesha mkoani Dodoma na mikoa jirani eneo  kati ya stesheni za reli ya kati za Gulwe na Godegode zimejaa maji na kufunika njia ya reli mkesha wa mwaka mpya wa 2014!.
Tokea juzi Januari  02, 2014 Wahandisi na mafundi wa kampuni za TRL na Rahco kwenye sehemu husika wakifanya tathmini  na kusimamia ukarabati wa maeneo mawili  reli  yaliyoharibika.
Kwa mujibu Mkururgenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Amani Kisamfu anayeongozwa kikosi kazi cha kukarabati amesema kazi ya ukarabati inafanywa usiku na mchana kuona huduma zinaanza mapema iwezekanavyo ikiwemo huduma ya  usafiri  wa treni za abiria uliopangwa kuanza tena hapo kesho Jumapili Januari 05, 2014.
Kutokana na dharura hii treni za kutoka Mpanda, Kigoma na Mwanza kuja Dar zimebadilishiwa muda na siku ya kuondoka hivyo basi,  badala ya kuondoka jana Ijumaa Januari 03, 2014 sasa zitaondoka kesho Jumapili Januari 05, 2014 saa 2 asubuhi.

Aidha taarifa  hii iwafikie wadau wote wa usafiri na huduma ya reli ya kati na kwamba uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza..

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Paschal Mafikiri.
TRL Makao Makuu,
Dar es Salaam.
Januari 04, 2014

No comments:

Post a Comment