Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma
Kikwete akipokewa rasmi na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Mheshimiwa Dkt. Seif Rashid, kwenye hoteli ya Serena alikoenda kufungua
mkutano wa majadiliano ya wadau kuhusu kutokomeza maambukizi ya virusi
vya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto tarehe 21.1.2014.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dkt. Seif Rashid (kulia) na Mheshimiwa Mama Zakhia Meghji, Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya WAMA, (kushoto), wakielekea kwenye chumba cha
mkutano.
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akifungua rasmi mkutano
wa siku moja wa majadiliano ya wadau kuhusu kutokomeza maambukizi ya
virusi vya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto uliofanyika kwenye
hoteli ya Serena tarehe 21.01.2014.
CHANZO MICHUZI BLOG
No comments:
Post a Comment