Timu ya
Manchester City jana iliibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya West Ham
United katika mzunguko wa raundi ya pili ya kombe la ''Capita One Cup''
na hatimaye kujihakikishia kucheza fainali ya kombe hilo itakayofanyika
March 2, 2014 katika uwanja wa Wembley, Manchester city inasubiri
mshindi kati ya Manchester united au Sunderland ambao watacheza leo
katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
Alvaro
Negredo aliifungia Manchester City magoli mawili (2) wakati Sergio
Arguero akimalizia goli la tatu na kuiwezesha Manchester City kuibuka na
ushindi wa magoli 3-0, kwa matokeo hayo Manchester City iliibuka na
ushindi kwa jumla ya magoli 9-0 kwa michezo yote miwili (Home and Away).
Itakumbukwa kuwa Manchester City waliibuka na ushindi wa magoli 6-0
dhidi ya West Ham United katika uwanja wake wa nyumbani ''Etihad''
Manuel
Pellegrini akuwachezesha wachezaji wake kama Yaya Toure, Vincent
Company, Pablo Zabaleta, David Silva na wengine wakati timu hiyo
ikichezesha wachezaji baadhi wanaowakilisha kikosi cha pili kama Boyata,
Lescott,Lopes, Garcia na wengine, pia kuna baadhi ya wachezaji mahiri
wanaowakilisha kikosi cha kwanza walitumika kuihakikishia Manchester
City ushindi kama vile Fernandinho, Alvaro Negredo, Sergio Aguero,
Nastasic, Clichy na Jesus Navas.
Mchezo ulikuwa na takwimu kama zinavyoonekana hapa chini.
Manchester
City itakutana na mshindi kati ya Manchester United au Sunderland mnamo
tarehe 2, March/2014 katika uwanja wa Wembley ili kumpata mbabe wa
kombe hilo la Capital One Cup.
Chanzo, skysports.com/uk
No comments:
Post a Comment