TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Baraza
la Habari Tanzania (MCT) kwa niaba ya Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za
Umahiri za Uandishi wa Habari Tanzania(EJAT) 2013, imeongeza muda wa
kuwasilisha kazi za kushindaniwa hadi Januari 21, 2014.Tarehe ya awali
ya kuwasilisha kazi hiyo ilikuwa Januari 15, 2014.
Muda
huo wa kuwasilisha kazi umeongezwa baada ya kuwepo kwa siku za
mapumziko zilizofuatana na ofisi kufungwa, jambo lililowafanya baadhi ya waandishi
washindwe kuwasilisha kazi zao kwa wakati. Vile vile hii ni fursa
nyingine kwa waandishi wanaotaka kushiriki kwenye EJAT2013. Hata hivyo
baada ya Januari 21, 2014 hakuna muda zaidi utakaoongezwa.
Kamati ya Maandalizi ya EJAT 2013 inaundwa na Mfuko wa Vyombo
vya Habari Tanzania (TMF), Johns Hopkins University, Taasisi ya Vyombo
vya Habari Kusini Mwa Afrika –Tawi la Tanzania (MISA-Tan), Chama cha
Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Chama cha Waandishi wa
Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Chama cha Waandishi wa Habari za
Mazingira (JET), Jukwaa la Wahariri (TEF), HakiElimu, AMREF, ANSAF,
BEST-AC, SIKIKA, Chama cha Waandishi wa Habari Dhidi ya Ukimwi ( AJAAT) na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT).
Kajubi D. Mukajanga
Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi ya EJAT 2013
No comments:
Post a Comment