Hii
inamfanya Binyavanga kuwa mmoja wa wafrika mashuhuri kujitokeza hadharani.
Matendo ya
kimapenzi kwa watu wa jinsia moja hayakubaliwi nchini Kenya, na nchi nyinginezo
za Afrika.
Alifichua
hali hii katika taarifa yake kupitia kwa mtandano wa kijamii wa Twitter
iliyowiana na siku ya kuzaliwa kwake.Ana umri wa miaka 43.
Hii inakujia
wakati ambapo kuna mjadala mkali nchini Kenya na katika baadhi ya mataifa ya
Afrika kuhusiana na suala la haki za wapenzi wa jinsia moja.
Hivi
karibuni, Nigeria ilipitisha sheria ambayo inatoa adhabu kali kwa makundi ya
watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, ilhali Rais wa Uganda alikataa
kuhalalisha mswada kama huo uliopitishwa bungeni.
Uamuzi wa
Binyavanga kujitokeza hadharani umepokelewa kwa hisia mbali mbali nchini Kenya.
Kunao waliompongeza ingawa baadhi wanahisi kuwa huenda jamii ikamnyanyapaa.
Binyavanga
aliwahi kushinda tuzo la mwanadishi bora zaidi Afrika la Caine mwaka 2002.
Watu
wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja nchini Kenya wanaweza kuadhibiwa kifungo
cha miaka kumi jela ikiwa watapatikana na hatia.
No comments:
Post a Comment