Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, January 4, 2014

Mwumbui; apewa tuzo kwa kumsindikiza kliniki mjamzito



Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal (kushoto) akimpa Elia Mwumbui tuzo ya heshima ya kuchangia kupunguza vifo vya mama wajawazito. Picha na Fedelis Felix 

Kwa desturi iliyojengeka nchini, wanaume wengi hawana utamaduni wa kuwasindikiza wake zao kwenda kliniki kupima ujauzito au kupeleka watoto.
Hali hii inatokana na mfumo dume uliojengeka au wanaume kuona aibu kufanya hivyo au kuhofia kuchekwa na wenzake.
Licha ya tatizo hilo kwa walio wengi, hali ni tofauti kwa Elia Mwumbui (26), yeye ni mmoja wa wanaume wanaofaa kuigwa kutokana na kuthamini akitekeleza kwa vitendo  uzazi wa mpango kwa kuhudhuria kliniki, akiambatana na mkewe.
Kwa kutekeleza hilo na kutambua mchango wake, Taasisi ya Madaktari Wahitimu wa Vyuo Vikuu vya Tanzania (TPHI), imemtunukia Mwumbui, Tuzo ya Heshima ya Kutambua Mchango wake, kwa kupunguza vifo vya wajawazito.


TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
“Sikujua kama ni raha kumsindikiza mke wangu kliniki, nimejifunza mengi ambayo kila mwanaume anatakiwa kumfanyia mke wake,” anasema Mwumbui
Mwumbui ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Matongo, Wilaya ya  Ikungi, mkoani Singida, aliwavutia watu wengi kutokana na mazingira anayoishi kijijini, kuamua kujitoa kwenda na mke wake kliniki, jambo ambalo ni nadra kuliona.
Dk Telesephory Kyaruzi, Mkurugenzi Mkuu wa THPI, anasema kuwa wameamua kutambua mchango wa Mwumbui katika kupunguza vifo vya wajawazito kutokana na wakati wote kuhudhuria kliniki pamoja na mke wake.
Dk Kyaruzi ambaye alimtunuku Mwumbui tuzo hiyo anasema  kuwa, ili mwanamke aweze kulea ujauzito na kujifungua salama, mwanaume ana mchango mkubwa, wenye kumhamasisha mwanamke hasa anapomwona  akimhudumia kwa vitendo kwani hujisikia vyema.
Tuzo hizo za heshima kwa kuwa mstari wa mbele kuboresha afya ya mama na mtoto nchini, zilizotlewa na THPI ziwatambua watu wanane.
Watu hao walitunukiwa tuzo hizo na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal mapema Novemba mwaka jana, lakini kivutio zaidi alikuwa Mwumbui.
Mara baada ya kuitwa kuchukua tuzo hiyo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Mwumbui alishangiliwa na umati wa watu ulihudhuria, huku baadhi wakiimba “Shemeji, ...shemeji, ...shemeji,’ kitendo kilichomfurahisha kila aliyekuwapo eneo hilo.CHANZO MWANAINCHI

No comments:

Post a Comment