Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, January 22, 2014

OBAMA KUKUTANA NA PAPA FRANCIS MARCH, 2014.

PAPA_NEW_6a010.jpg
Rais wa Marekani Barack Obama atakutana na Papa Francis huko Vatikan wakati wa ziara yake ya wiki moja Ulaya iliyopangwa kufanyika mwishoni mwa Machi.
White House inasema rais Obama anatarajia kuzungumza na Papa Francis kuhusu mtizamo wao unaolingana katika kupambana na umasikini na tofauti ya kipato inayoendelea kuongezeka.
Mkutano huo umepangwa kufanyika Machi 27 .Wakati akiwa Roma rais Obama anapanga kukutana na rais wa Italia Giorgio Napolitano na waziri mkuu Enrico Letta.
Kiongozi huyo wa Marekani ataanza ziara yake ya Ulaya huko The Hague Uholanzi ambako atashiriki katika mkutano wa usalama wa nyuklia ulioandaliwa na serikali ya Uholanzi.
Chanzo, voaswahili.com

No comments:

Post a Comment