skip to main |
skip to sidebar
MAN UNITED USO KWA USO NA SUNDERLAND LEO.
Timu ya Manchester United leo itaivaa
timu ya Sunderland katika uwanja wake wa nyumbani wa Old Trafford katika
mzunguko wa pili wa nusu fainali ya kombe la Capital One Cup, mshindi
kati ya Manchester United au Sunderland atakumbana na Manchester City
ambayo imeshafuzu hatua ya fainali itakayochezwa katika uwanja wa
Wembley.
Sunderland iliutumia vizuri uwanja
wake wa nyumbani ''Stadium of Light'' baada ya kuitandika timu ya
Manchester United magoli 2-1, hivyo timu ya Manchester United
italazimika kushinda mchezo huo ili kutetea nafasi yao ya kutinga katika
fainali hizo.
mechi hii itachezwa mida ya 10:45 PM kwa masaa ya afrika mashariki.
Chanzo, goal.com
No comments:
Post a Comment