RPC Mungi
..................................................
NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA
JESHI
la polisi mkoani Iringa linawashikilia watu wawili kwa makosa mawili
tofauti likiwemo la Wilson Mbilinyi (25) mkazi wa Barabara mbili kata ya
Makorongoni wilaya ya Iringa kukutwa na madawa ya kulevya.
Akizungumza
na mtandao wa www.matukiodaima.com ofisini kwake Kamanda wa polisi mkoa
wa Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo
lililotokea januari 16 majira ya saa 5 kamili asubuhi.
Mungi alisema mtuhumiwa huyo alikutwa na kete 15 zinazozaniwa kuwa ni madawa ya kulevya aina ya kokeini.
Wakati
huohuo jeshi la polisi mkoani Iringa lilimkamata raia wa Ethiopia
Dasala Halute (20) kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.
Kamanda
Mungi alisema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 16 januari mwaka huu
majira ya saa 3:30 usiku maeneo ya Ipogolo kata ya Ruaha.
Credit: www.matukiodaima.com
No comments:
Post a Comment