Msimamizi
wa Uchaguzi Jimbo la Kiembesamaki Bwa. Suluhu Ali Rashid, akitowa
maelezo kwa mgombea wa CCM alipofika kuchukua fomu ya kugombea
Uwakilishi katika Ofisi za Tume Maisara.
Akionesha fomu zake baada ya kukabidhiwa na Afisi wa Tume ya Uchaguzi
MGOMBEA
nafasi ya Uwakilishi katika Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki
Bwa,Mahmoud Thabit Kombo, akikabidhiwa Fomu ya kugombea nafasi hiyo na
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kiembesamaki Suluhu Ali Rashid,
makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Maisara
Mgombea
wa Uwakilishi katika uchaguzi mdogo wa jimbo la kiembesamaki Bwa Mahmoud
Thabit Kombo akionesha Fomu zake za kugombea nafasi hiyo ya Uwakilishi
ya Jimbo la Kiembesamaki baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi
Mgombea
wa Chama cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki
Bwa. Mahmoud Thibit Kombo akishindikizwa na Wanachama wa CCM wa jimbo la
Kiembesamaki baada ya kuchukuwa Fomu za kugombea Uwakilishi kupitia
uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika mwazoni mwa mwezi wa Febeary 2014,
kuziba nafasi ilioachwa wazi na Mhe. Mansoor Yussuf Himid aliyevuliwa
Uwanachama wa CCM na Chama chake mwaka jana.
Mgombea
wa Chama cha Mapinduzi Bwa Nahamoud Thabit Kombo akiondoka katika Ofisi
za Tume ya Uchaguzi kwa kushindikizwa na wapanda Pikipiki kuelekea
katika Ofisi za CCM tawi la Kiembesamaki kwa mazungumzo na Wanachama wa
CCM wa Jimbo la Kiembesamaki.Picha Zote na Othman Mapara-Zanzibar
No comments:
Post a Comment