Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, January 15, 2014

Rais Kikwete awaapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia na Kamisha wa Tume ya Usuluhishi,ikulu jijini dar leo

Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt.Aziz Ponary Mlima akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Kamishna wa Tume ya usuluhishi na uamuzi Bwana Jafari Omari akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wateule aliowaapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kushoto ni Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Bwana Jafari Omari na kulia ni Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt.Aziz Ponary Mlima .Picha na Freddy Maro wa Ikulu.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo asubuhi amewaapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia na Kamishna wa Tume ya usuluhishi na Uamuzi.Walioapishwa leo katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam ni Dkt.Aziz Ponary Mlima anayekuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia na Bwana Jafari Omari anayekuwa Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi.

No comments:

Post a Comment