Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dk. Jakaya
Kikwete, amewapandisha cheo maafisa wakuu kutoka Kanali kuwa Brigedia
Jenerali.
Taarifa
ya Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi, ilieleza jana
kuwa Rais amezingatia Kanuni za Majeshi ya Ulinzi, Aya ya 7.01 Kifungu
cha 13 Juzuu ya Kwanza (Utawala).
Maafisa
Wakuu hao ni Kanali Denis Raphael Janga, Kanali Jason Nestor Musikula,
Kanali Jackson King Mrema, Kanali Martin Amos Kemwaga, Kanali Joseph
Cosmas Chengelela, Kanali Martin Nikubuka Mwankanye, Kanali Harold
Kidundi Mziray, Kanali Emmanuel Peter Kapesa na Kanali Mwita Wambura
Isamulyo.
Wengine
ni Kanali Francis Asilia Njau, Kanali Pendo Uledi Kamungwele, Kanali
Moses Adolph Shinyambala, Kanali Ibrahim Abdarahamani Kimario, Kanali
Michael Garo Luwongo, Kanali Nelson Hosea Msanja, Kanali Blasius Kalima
Masanja, Kanali Aloyce Damian Mwanjile, Kanali Rajabu Goma Hanti, Kanali
Ignas Beatus Mubofu na Kanali Dominic Basil Mrope.
Pia
wamo Kanali Hamis Issa Majumba, Kanali Salehe Omari Semtaua, Kanali
Henry Sweko Kamundo, Kanali Sylivester Msafiri Minja, Kanali John
Bangantagoka Bishoge, Kanali Anselm Shigongo Bahati, Kanali Robinson
Mboli Mwanjela na Kanali Kaisy Philip Njelekela.
Mnadhimu
Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali
Samueli Ndomba kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis
Mwamunyange, aliwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuleta tija
na maendeleo katika JWTZ na Taifa kwa ujumla.
Aidha, Luteni Jenerali Ndomba alisisitiza kusimamia nidhamu na ueledi.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment